TUTAIRARUA KIYOVU KIULAIIIIIN-MILOVAN

KOCHA mkuu wa Simba Milovan Cirkovic amesema ameshamaliza kazi yake ya kuinoa kikosi chake tayari kwa mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa Afrika (CAF) dhidi ya Kiyovu Sport ya Rwanda utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Milovan amesema kupitia mabadiliko aliyoyafanya katika kikosi chake anaminani wachezaji wake hawatamuangusha uwanjani kwa kuhakikisha wanashinda na hatimaye kusonga mbele.
Aidha, Milovan amejivunia uwepo wa wachezaji wake Amir Maftah na Haruna Moshi 'Boban' ambao hawakucheza mechi ya mwanzo iliyopigwa wiki mbili zilizopita huko Rwanda na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Comments