TOTO AFRICANS YAAPA KUIADHIRI YANGA

LICHA ya kudaiwa kuwa na 'undugu'  na mabingwa watetezi wa Yanga, timu ya Toto Africans ya jijini Mwanza imeapa kuifunga Yanga katika mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania Bara utakaopigwa Aprili 15 kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kocha wa Toto Africans Athuman Bilal amesema anahitaji kushinda mchezo huo ili kujipatia pointi tatu muhimu zitakazowaweka katika nafasi nzuri ya kuepukana na kushuka daraja.
"Pia tunataka kuonyesha kuwa hatuna undugu na Yanga, kwa sasa kikosi changu kipo kwenye maandalizi makali ya mchezo huo na mingine ya Ligi,"Alisema.

Comments