KUNDI la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Family la
jijini Dar es Salaam ni miongozi mwa burudani
zitakazokuwepo kwenye bonanza la vyombo vya habari linaloandaliwa na Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA).
Bonanza hilo litafanyika kesho katika ukumbi wa Msasani Beach
Club, Dar es Salaam ,
huku TASWA ikiamini litakuwa bora na la uhakika.
Licha ya Wanaume Family, burudani nyingine itakuwa bendi ya muziki wa dansi ya
FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, ambapo wadhamini ni Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL).
Tunataka bonanza la mwaka huu liwe la aina yake kuanzia
burudani, michezo na mambo mengine yawe ya aina yake.
Bonanza litaanza saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku,
ambapo baadhi ya michezo itakayoshindaniwa ni soka ya ufukweni, netiboli, wavu,
mbio za magunia, mbio meta 100, kuruka kichura, kuvuta kamba, kucheza muziki na
michezo.
Mgeni rasmi katika bonanza hilo atakuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta.
Lengo la bonanza ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari
bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine, ili
kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja na huwa linafanyika mara moja kwa
mwaka, likiandaliwa na TASWA
George John
Mwenyekiti Kamati ya Bonanza
23/03/2012
Comments
Post a Comment