TINGATINGA LABOMOLEA WAVAMIZI 'SIMBA SC ARENA'


KLABU ya soka ya Simba kwa kushirikiana na jeshi la polisi juziwameendesha zoezi la uvunjaji wa nyumba zilizojengwa katika eneo laUwanja wao huko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaj Ismail Aden Rage alisema jana kwamba wavamizi hao walijenga nyumba  tatu ambazo zilikuwa katika hatua za mwisho wakati wakijua eneo hilo ni mali ya Simba.
Alisema baada ya kuwauliza watu wanaodaiwa kuhusika na umiliki wanyumba hizo kila mtu alijitetea anavyojua ambapo kuna mmoja alidai
kuuziwa eneo hilo na mwingine alidai kuwa alipatiwa na babu yake.
“Mimi nashangazwa na wavamizi hawa sijui wanajiamini nini…baada ya kubaini uvamizi huo tulitaarifu polisi na wakafanya uchunguzi wao na sisi tukatoa vithibitisho na juzi kuliendeshwa zoezi la uvunjaji wa
nyumba hizo,”Alisema.
Rage alisema wakati wowote wataalamu wa kampuni ya  Petroland yanchini Uturuki  wanatarajiwa kutua na kuanza mchakato wa kuelekeaujenzi wa uwanja huo ambapo utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000, pia utazungukwa na vitega uchumi
vya aina mbalimbali..

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHMarch 10, 2012 at 7:52 AM

    TAMTHILIA YETU YA UWANJA WA KISASA WENYE MADUKA INAENDELEA,ADEN...NAMPENDA SANA KAKANGU YULE ANAWAPATIA SANA SIMBA...!

    WATAALAM WANAKUJA KUANZA MCHAKATO WA KUELEKEA UJENZI...

    CHANGA LA MACHO LA TV YA SIMBA KUMBE NI TV SHOW TUMEELEZWA NI MCHAKATO KUELEKEA SIMBA KUMILIKI TV YAKE,HII MIKAKATI NA MICHAKATO ADEN ITAKAMILIKA WAKATI MUDA WAKE WA KUKAA MADARAKANI
    UMEKWISHA,NI STRATEGY TU YA KUITAWALA SIMBA KWA AMANI NA UTILIVU

    ReplyDelete

Post a Comment