TIKETI 'DIAMONDS ARE FOREVER' ZIMEKWISHA

TIKETI kwa ajili ya onyesho maalum lililobatizwa kama 'Diamonds are Forever' litakalofanyika kesho kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam likiongozwa na msanii Nasib Abdul 'Diamond' zimemalizika.
Mmoja ya waratibu wa onyesho hilo Babu Tale amesema kwamba licha ya watu kuhitaji zaidi tiketi hizo hakutakuwa na tijketi za ziada kwani onyesho hilo haliitaji watu wengi.
"ONysho hilo la kwanza lenye mlengo wa kuwapa burudani baadhi ya watu wasiopenda vurugu na msongamano , hivyo sidhani kama itakuwa busara kujaza watu ukumbini,"Alisema Babu Tale.
Aidha kampuni ya The Unity ambayo imeandaa onyesho hilo kwa kiingilio cha sh.50,000 kwa kila kichwa litakuwa likifanyika mara moja kwa mwaka tu likihusisha msanii anayefanmya vema kwa mwaka husika.

Comments