THABEET KATIKA TIMU YA TATU NBA


Hasheem Thabeet katikati na jezi ya timu yake mpya
MCHEZAJI wa kulipwa wa mpira wa kikapu wa Tanzania, Hasheem Thabeet amechukuliwa
na klabu ya Portland Trail Blazers inayoshiriki kwenye Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA) kutoka klabu ya Houston Rockets.
Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mitandao mbalimbali ya intaneti, Portland Trail Blazers imefanikiwa kumnyakua Mtanzania huyo kutoka Rockets kwa kubadilishana na mchezaji mwingine Marcus Camby, jana ambayo ilikuwa siku ya mwisho iliyowekwa na NBA kwa ajili ya
klabu zinazocheza ligi hiyo kufanya utaratibu huo wa kubadilishana wachezaji.
Mlinzi Jonny Flynn, pia amejiunga na klabu ya Portland Trail Blazers kama sehemu ya utaratibu huo, Thabeet ambaye sasa amechukuliwa na Blazers kabla alichukuliwa na Houston Februari mwaka jana, akitokea Memphis na alifanikiwa kuichezea Rockets mechi tano pekee
katika msimu huu wa ligi.
“Tunatazamia kuwa yale yatakayofanywa na Jonny pamoja na Thabeet yanaweza kuleta mafanikio katika timu yetu na pia tunamshukuru Marcus kwa mchango alioutoa kwa kipindi cha misimu mitatu aliyokuwa nasi na tunamtakia kila la heri huko alikoenda,” alisema Kaimu Meneja Mkuu wa Blazers Chad Buchanan.
Katika michezo 120 ya misimu mitatu akiwa na klabu za Memphis na Houston, Thabeet mwenye umri wa miaka 25, ana wastani wa pointi 2.2, na jumla ya dakika 10.7 pamoja na rebaundi 2.7.

Comments

  1. Of course anaenda mashambani huko Oregon....nyie waandishi wa habari wa bongo mnampa sifa sana...hii ni NBA siyo college Basketball.....

    ReplyDelete

Post a Comment