TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UCHAGUZI
WA VIONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA
WA KAGERA (KRFA).
TAREHE
21/03/2012
1.
Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) linawajulisha wadau wa soka kwamba uchaguzi wa viongozi
wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa Kagera ulifanyika tarehe 17 Machi 2012, Bukoba
mjini kama ulivyokuwa umepangwa. Uchaguzi huo ulifanyika kwa mujibu wa Katiba ya
KRFA na Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF.
2.
Viongozi
waliochaguliwa kwenye Kamati ya Utendaji ya KRFA ni hawa wafuatao:
(i)
Mwenyekiti:
Ndg. Jamal E. Malinzi
(ii) Makamu Mwenyekiti:
Ndg. Alex Raphael
Gashaza
(iii) Katibu Mkuu:
Ndg. Salum H.
Umande
(iv) Mweka Hazina:
Ndg. Adolf Martin Mahuguli
(v) Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF:
Ndg. Peregrinius A. Rutayuga(vi) Mjumbe- Mwakilishi wa Vilabu: Ndg. Didas David Zimbihile
(vii) Wajumbe- Kamati ya Utendaji: - Ndg. Abubakari Kazinja
- Ndg. Dionise Magezi
- Ndg. Ezekiel Geofrey Samson
3.
TFF inawashukuru
wadau wa soka Mkoani Kagera, hususan, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KRFA na Kamati
ya Uchaguzi ya KRFA kwa kuheshimu na kuzingatia Katiba ya KRFA,
Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na kwa ushirikiano mkubwa
walioutoa kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, hivyo kufanikisha kufanyika kwa
uchaguzi wa KRFA kama ulivyopangwa. Ni matumaini ya TFF kuwa wadau wa soka
Mkoani Kagera wataendelea kushirikiana na TFF kuendeleza soka katika Mkoa wa
Kagera.
Sunday
Kayuni
KAIMU
KATIBU MKUU
Comments
Post a Comment