TFF KUJADILI MGOMO WA SIMBA SC


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) linatarajia kujaidili kauli ya kugomea wachezaji wake kuichezea timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ iliyotolewa juzi na klabu ya soka ya Simba.
Simba kupitia kwa mwenyekiti wake Alhaj Isamil Aden Rage alisema juzi kwamba watafikia hatua hiyo kutokana na TFF  kutothamini mchango wa vilabu vya Ligi kuu ambavyo ndiyo chimbuko la Stars lakini badala yake imekuwa ikiwaonea katika mapato.
Rage alitolea mfano wa wachezaji wao waliokuwa wakiitumikia Stars kurudishwa siku mbili kabla ya mechi yao ya kombe la shirikisho dhidi ya Kiyovu ya Rwanda na kusema kuwa kama TFF ingekuwa inawajali ingeomba kusogezwa kwa mchezo huo. 
Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema leo kwamba  kauli ya Rage si nzuri na inapaswa kukemewa kwani Stars ni timu ya Taifa na si mali ya TFF,m hivyo watalijadili hilo kabla ya kulitolea maamuzi. 
Aidha, Wambura alisema TFF imelazimika kuikata Simba mil.5 kama fidia ya uharibifu wa vbiti 152 uliofanywa na mashabiki wakati wa mchezo wao dhidi ya Kiyovu jumapili iliyopita kutokana na ukweli kwamba mchezo huo uliwahusu wao.

Comments