TEVEZ AANZA KUNOGA, KUKIPIGA NA CHELSEA MACHI 19

MSHAMBULIAJI Carlos Tevez amekata weight ile mbaya tangu arudi kazini Manchester City mwezi uliopita na sasa yuko tayari kufanya mamboz kuipuiga tafu timu yake katika vita ya ubingwa wa Ligi Kuu.
Mshambuliaji huyo wa Kiargentina aliifungia bao timu yake katika akiichezea kikosi cha wachezaji wa akiba dhidi ya Bolton usiku wa jana, hiyo ikiwa mechi ya kwanza kuonekana hadharani akiwa na jezi ya City baada ya zaidi ya miezi mitano.
Katika dakika 66 alizocheza kwenye Uwanja wa Hyde, akifuatiliwa na Kocha Msaidizi wa City, Brian Kidd Ofisa Utawala, Brian Marwood, Tevez alionekana mwepesi zaidi ya alivyokuwa mechi iliyochezwa milango imefungwa dhidi ya Preston wiki iliyopita.
Na City iko tayari kumpokea tena baada ya mavitu adimu aliyofanya jana.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alirejea kwenye klabhu hiyo akiwa hayuko fiti na baada ya kuimarika anaweza kucheza mechi dhidi ya Chelsea, Machi 19.
Tevez, ambaye alikaribishwa na mashabiki wapatao 1000 wa City, anatarajiwa kusafiri na kikosi hicho cha wachezaji wa akiba katika mchezo mwingine wa kirafiki wiki ijayo dhidi ya NEC Nijmegen nchini Uholanzi.
Tevez alikorofishana na kocha wa City, Roberto Mancini baada ya kugoma kuingia kucheza dakika za lala salama mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich, Septemba mwaka jana.
Lakini baadaye aliomba radhi kwa Mtaliano na sasa anatarajiwa kurejea dimbani kwenye kikosi cha vinara hao wa Ligi Kuu muda si mrefu.

Comments