TENGA:ADHABU YA WACHEZAJI YANGA NI SAHIHI


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limesema adhabu walizopewa wachezaji wa klabu ya soka ya Yanga ni sahihi kwani kumpiga mwamuzi ni utovu wa nidhamu.
Hatua hiyo inafuatia Yanga kulalamikia adhabu ya vifungo na faini waliyopewa wachezaji wake watano kutokana na kumpiga mwamuzi Israel Nkongo mmwishoni mwa wiki iliyopita wakati Yanga ilipocheza na Azam Fc katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwewnye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam .
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Rais wa TFF Leodger Tenga alisema wachezaji hao waliadhibiwa kwa mujibu wa sheria na Kanuni za soka na mchezaji yoyote atakayeonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu ataadhibiwa kwa mujibu wa kanuni.
“Wachezaji kumpiga mwamuzi si tu kinyume cha sheria ni utovu wa nidhamu…haya mambo yalikuwa zamani lakini kwa sasa mambo hayo yanatakiwa kufanywa katika mechi za mchangani lakini si kwa wachezaji ambao tunateghemea siku moja wakacheze soka la kulipwa nje ya nchi,”Alisema Tenga. 

Comments