TAARIFA TOKA SIMBA SC HII LEO


Adobe Systems SIMBA SPORTS CLUB                         
P.O.BOX 15318 | TEL+255 222183330 |FAX +255 222183330 |MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET | DAR ES SALAAM | TANZANIA | EMAIL   simbasportsclub@yahoo.com|
WEBSITE www.simba.co.tz| AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA
                                                                                                 29/03/2012

                       TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wasalaam.

KLABU ya Simba inapenda kutoa taarifa zifuatazo kwa vyombo vya habari.

SUALA LA MAFISANGO

Mchezaji Patrick Mafisango amesimamishwa kuichezea Simba kwa muda usiojulikana baada ya jana kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu kwa waajiriwa wengine wa klabu na klabu kwa ujumla katika kambi ya timu iliyopo Bamba Beach jijini Dar es Salaam.

Kutokana na utovu huo wa nidhamu, Mafisango hatasafiri na timu kwenda Algeria. Uongozi tayari umeamuandikia barua ya kutaka ajieleze kwa makosa yake na maamuzi kamili yatatolewa mara timu itakaporejea kutoka Setif kwenye mechi ya marudiano.

SUALA LA MGOMO

Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti wiki hii kuwa wachezaji wa Simba wapo katika mgomo kutokana na kutopewa stahili ya mgawo wao wa mapato kwenye mechi dhidi ya Setif.

Taarifa hizi hazina ukweli wowote. Kwanza, wachezaji karibu wote wa Simba isipokuwa wale ambao taarifa zao zinajulikana kwa uongozi wako kambini.

Wachezaji wa Simba wasingeweza kugomea mgawo huo kwa sababu mikataba yao inaeleza wazi kuwa wanatakiwa kulipwa asilimia ya mapato ya mechi kwenye mechi za ndani na si zile za kimataifa.

Tunakaribisha waandishi wa habari na vyombo vyao waje kambini Bamba na wajionee wenyewe kwa macho yao kama kuna hicho kinachoitwa MGOMO.

Comments