SWANSEA UTAWATAKA!



KLABU ya Swansea City iliweza kujipenyeza katika nafasi ya nane ya Ligi Kuu ya England, baada ya Gylfi Sigurdsson kuongezea mabao mawili zaidi ambayo yaliiwezesha timu yake kujihakikishia ushindi ilipocheza na Fulham, na kupata ushindi wa tatu mfululizo katika mechi ya ligi kuu.
Kiungo huyo wa kati alifunga bao la pili katika kipindi cha pili, baada ya kuupokea mpira kutoka kwa Wayne Routledge.
Joe Allen alikamilisha utaratibu huo wa kuondoka na ushindi kutoka Craven Cottage, kupitia mkwaju kutoka yadi 18.
Kinyume na matazamio ya mashabiki wengi, wachezaji wa Fulham walishindwa kuvuma, kama ilivyotazamiwa, na ngome yao ikiwa ni dhaifu mno.
Swansea, tangu kuishinda Manchester City, imekuwa ni timu ya nne kupata ushindi katika uwanja wa Fulham msimu huu.
Huo ulikuwa ni ushindi wa nne ugenini msimu huu kwa timu hiyo ya Wales.
Timu hiyo imewathibitishia wote kwamba itaweza kusalia katika michuano ya ligi kuu ya Premier.
Huku Kocha Martin Jol akishindwa kuiokoa timu yake, Wigan nao walijipata katika matatizo katika mechi ya pili ya Jumamosi, kwani wanaendelea kuwa katika nafasi ya mwisho katika ligi ya msimu huu, baada ya kukosa kuzitumia vyema nafasi za kufunga mabao, na hatimaye kutoka sare ya 1-1 walipocheza na West Brom.
James McArthur aliiwezesha Wigan kutangulia kufunga katika kipindi cha pili, lakini Paul Scharner aliiwezesha Albion kusawazisha.
Iwapo Wigan wangelipata ushindi, basi wangelifanikiwa kujinusuru kuondolewa kutoka ligi kuu, lakini kabisa walishindwa kuzitumia nafasi zilizojitokeza.

Comments