SUNDERLAND YAKWAMA KWA EVERTON


Beki wa Sunderland Wayne Bridge (kushoto) akigombea mpira na kiungo wa Everton, Tim Cahill (kulia) 
BAO la Tim Cahill kipindi cha kwanza limeipeleka Everton katika mechi ya marudiano ya Kombe la FA dhidi ya Sunderland baada ya timu hizo za Ligi Kuu kutoka sare ya 1-1 kwenye Robo Fainali.
Phil Bardsley alifunga bao la kuongoza kwa Sunderland dakika ya 12 kwenye Uwanja wa Goodison Park kwa shuti la mbali, lakini Cahill akasawazisha dakika 11 baadaye.
Tottenham inaikaribisha Bolton baadaye katika mchezo mwingine wa Kombe la FA wakati kwenye Ligi Kuu kuna mechi mbili kati ya Fulham vs. Swansea na Wigan vs. West Bromwich Albion.

Comments