STARS, WAMACHINGA WAINGIZA MIL.64


Mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika- AFCON 2013 kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) iliyochezwa jana (Februari 29 mwaka huu) imeingiza sh. 64,714,000.

Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 16,776 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo lililochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Sehemu iliyoingiza watazamaji wengi ilikuwa viti vya bluu na kijani ambapo 14,403 walikata tiketi kwa kiingilio cha sh. 3,000 kwa kila mmoja. Viingilio vingine katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C, sh. 15,000 viti vya VIP B wakati VIP A iliyoingiza watazamaji 91 kiingilio kilikuwa sh. 20,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ni kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ilikuwa sh. 9,871,627, gharama ya kuchapa tiketi sh. 4,500,000, malipo kwa waamuzi wane na kamishna wa mchezo huo sh. 12,180,000 na ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000.

Malipo kwa Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000, maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000 wakati asilimia 20 ya gharama za mchezo ni sh. 6,682,475.

Mgawo mwingine ni asilimia 10 ya uwanja sh. 3,341,237, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,670,136 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 21,718,042.

Comments