SIMBA YAWAFUATA MAAFANDE WA DODOMA

WEKUNDU wa Msimbazi Simba wameondoka jijini Dar es Salaam leo kwenda Dodoma tayari kwa mechi yao ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara dhidi ya maafande wa Polisi Dodoma itakayopigwa keshokutwa katika dimba la Jamhuri mjini Dodoma.
Simba inayoongoza ligi hiyo kwa pointi 41 imepania kumalizia hasira zake kwa maafande hao baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Toto African ya Mwanza jana.

Comments