SIMBA YATAKATA TAIFA, AZAM NAYO BALAAA

SIMBA SC imejiimarisha kileleni mwa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Ushindi huo, unaifanya Simba ifikishe pointi 40 baada ya kucheza 18, sasa inawazidi mabingwa watetezi, Yanga kwa pointi tatu. Yanga inacheza mechi yake ya 18 ya Ligi Kuu na Azam FC Jumamosi.
Mabao ya Simba katika mchezo wa leo yalitiwa kimiani na kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa  Mafisango dakika ya 25 na dakika ya 89 kwa penalti, baada ya kiungo Shomary Kapombe kufanyiwa kwenye eneo la hatari na beki David Luhende. Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emanuel Arnold Okwi aliifungia Simba bao la tatu katika dakika ya nne baad aya kutimu dakika 90 za kawaida za mchezo.
Bao la Kagera ambalo lilifanya mchezo uwe 1-1 lilifungwa na Themi Felix dakika ya 57.
Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu, Azam FC waliifunga Coastal Union ya Tanga mabao 3-0, wafungaji John Bocco 'Adebayor' mawili na lingine Kipre Herman Tchecthe.

Comments