SIMBA YATAJA WANAOKWENDA ALGERIA

JUMA Nyosso ametemwa kwenye kikosi cha kinachoondoka Jumatatu Alfajiri kwenda Algeria kikipitia Misri kwa sababu ameumia kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo dhidi ya African Lyon, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Habari kutoka ndani ya kambi ya Simba zimesema kwamba, wachezaji watakaoondoka ni Juma Kaseja, Derick Walullya, Shomary Kapombe, Kelvin Yondan, Jonas Mkude, Salum Machaku, Patrick Mafisango, Patrick Sunzu, Haruna Moshi ‘Boban’, Emanuel Okwi, Victor Costa, Uhuru Suleiman, Ally Mustafa ‘Barthez’, Amir Maftah, Mwinyi Kazimoto, Obadia Mungusa na Ramadhani Singano.
Mbali na Nyosso, Juma Jabu pia ni mgonjwa sambamba na Gervais Kago.
Aidha, pamoja na Simba kushinda mabao 2-0, lakini imebaini pengo la kiungo wake wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango iliyemsimamisha jana kwa muda usiojulikana.
Kuelekea mechi ya marudiano na ES Setif mwishoni mwa wiki ijayo, Simba lazima iwe na kiungo mtukutu kutoka Rwanda, ambaye aliwashinda Azam FC wakamtua Msimbazi bila dai lolote.
Habari za ndani kutoka Simba ambazo bongostaz imezipata zimesema kwamba, uongozi wa Simba ulilazimika kumuita Mafisango na kumpa onyo kali juu ya tabia zake na kumrejesha kambini Bamba Beach, Kigamboni tayari kwa safari ya Algeria.
“Mafisango amerejeshwa na anaondoka na timu kwenda Algeria usiku huu,”kilisema chanzo hicho kutoka Simba.
Bahati nzuri ni kwamba Mafisango alisimamishwa wakati tayari amekwishakabidhi pasipoti yake kwa uongozi kwa ajili ya kushughulikiwa viza ya safari ya kwenda Algeria.




Comments

  1. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHApril 1, 2012 at 12:33 AM

    bonge la weakness,eti mafisango tena anasafiri na timu,this means mafisango ni mkubwa kuliko kocha mkubwa kuliko club,mkubwa kuliko meneja nyagawa..!hii inanikumbusha ile hadithi ya mafisango na kocha wa azam mbrazil,hivi mafisango kwanini anaogopwa????ana nini cha ajabu hasa?


    mdau wa bomba,revere,boston,massachussetts.

    ReplyDelete

Post a Comment