SIMBA YAPANGA KUGOMEA MECHI ZA UWANJA WA TAIFA


KLABU ya soka ya Simba imetishia kugomea kucheza mechi zake katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, pia  kuzuia wanachama wake kuingia uwanjani, kutokana na  uonevu wanaofanyiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika mchakato mzima wa mapato ya mlangoni. 
Hatua hiyo inafuatia juzi TFF kuikata Simba mgao wake wote wa shilingi mil.3.5 ilioupata kupitia mapato ya mchezo wao wa ligi kuu baina yao na Kagera Sugar ya Kagera kwa madai ya fidia ya shilingi mil.tano wanazotakiwa kulipa baada ya wanaodaiwa mashabiki wa Simba kuharibu viti vya uwanja huo katika mechi baina ya Simba na Kiyovu iliyofanyika jumapili iliyopita. 
Mwenyekiti wa Simba  Alhaj Ismail Aden Rage amesema leo  kwamba wanashangazwa na uonevu wa wazi unaofanywa na TFF , kwa kuwa uwanja huo si mali yao  na wamekuwa wakilipa fedha nyingi kabla ya mchezo kama tahadhari kwa uharibifu wowote utakaotokea lakini haijulikani fedha hizo zinakwenda wapi. 
“Mfano mechi yetu na Kagera Sugar juzi mapato yalikuwa mil.24  na baada ya makato ya mamlaka mbalimbali zilibaki mil.7 na vilabu kugawana hivyo kila timu kupata mil.3.5, huu ni unyonyaji kabisa kwani pamoja na vilabu kugharamika kwa fedha nyingi kwenye maandalizi lakini mwisho wa siku wanakuja kufaidika watu wasiochangia mapato yoyote,”Alisema

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHMarch 8, 2012 at 11:51 PM

    Aden anachotakiwa yeye na uongozi wake sio kulia lia bali wawape semina elekezi washabiki wao kukaa kistaarabu uwanjani,na waace mchezo wa kuonyesha furaha za ushindi kwa kung'oa viti kwani mwisho wa siku kunaigharimu club,zipo njia nyingo za kushangilia ushindi,yanga bomba wanaweza kuwapa somo la ushangiliaji kama wataombwa na uongozi wa simba kwa barua rasmi.

    mdau wa bomba,revere masachussetts usa

    ReplyDelete

Post a Comment