SIMBA, YANGA VITANI LEO



MAHASIMU wa jadi nchini timu za Simba na  Yanga leo zitaendeleza harakati za kuwaniubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara ambapo watashuka katika viwanja viwilitofauti nchini.
Wakati Simba inayoongoza ligi hiyo kwa pointi 41  itashuka katika dimba la  Jamhuri mjini Dodoma kukwaana na maafande wa PolisiDodoma,  mabingwa watetezi Yanga wataikaribishaAfrican Lyon katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga yenye pointi 37 itacheza mechi ya leo bila nyotawake kadhaa tegemeo ambao wamefungiwa na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kwanyakati tofauti kutokana na vurugu katika mchezo wao na Azam Fc mwishoni mwawiki, huku pia ikiwa na machungu ya kufungwa mabao 3-1 katika mchezo huo.
Kwa mantiki hiyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa naushindani mkubwa kwani Yanga itahitaji kupoza machungu ya kupoteza mchezouliopita na hatimaye kujipatia pointi tatu muhimu ambazo zitawaweka kwenyemazingira mazuri katika kuelekea kutetea ubingwa wao.Lakini Yanga hataikishindinda itaendelea kubaki nafasi ya tatu kwani  Azam Fc inayoshika nafasi ya pili ina pointi 41.
Hata hivyo, Lyon nayo hawatakubali kirahisi kufungwa naYanga kwani nayo inazihitaji pointi tatu ili kujipandisha katika msimamo waligi hiyo ambapo kwa sasa inashikilia nafasi ya 10 ikiwa na pointi 18.
Kwa upande wa Simba, watashuka wakiwa na ari na kasizaidi ya kutaka kurekebisha matokeo yao ya sare ya bila kufungana na Toto African mwishoni mwa wiki hivyo kuwafanya kuwa na kibarua kigumu cha kuhakikishawanapata pointi tatu za ugenini ili waendelee kukalia kiti sambamba nakuchochea ndoto zao za kutwaa ubingwa.
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)limetaja viingilio vya mechi ya Yanga na Lyon itakayoanza kurindima saa 10.30jioni ambapo watakaokaa viti vya bluu na kijani watalipa  3,000, watakaokaa viti vya randi ya chungwawatalipa shilingi  5,000, huku watakaokaaVIP C na B watalipa shilingi sh. 10,000na VIP A watalipa shilingi 15,000.

Comments