SIMBA YAMREJESHA MAFISANGO, NYOSSO, YONDAN MAJERUHI

MECHI ya leo dhidi ya African Lyon pamoja na Simba kushinda mabao 2-0, lakini imebaini pengo la kiungo wake wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango iliyemsimamisha jana kwa muda usiojulikana.
Kuelekea mechi ya marudiano na ES Setif mwishoni mwa wiki ijayo, Simba lazima iwe na kiungo mtukutu kutoka Rwanda, ambaye aliwashinda Azam FC wakamtua Msimbazi bila dai lolote.
Habari za ndani kutoka Simba zimesema kwamba, uongozi wa Simba ulilazimika kumuita Mafisango na kumpa onyo kali juu ya tabia zake na kumrejesha kambini Bamba Beach, Kigamboni tayari kwa safari ya Algeria.
“Mafisango amerejeshwa na anaondoka na timu kwenda Algeria usiku huu,”kilisema chanzo hicho kutoka Simba.
Bahati nzuri ni kwamba Mafisango alisimamishwa wakati tayari amekwishakabidhi pasipoti yake kwa uongozi kwa ajili ya kushughulikiwa viza ya safari ya kwenda Algeria.
Simba itaondoka na kikosi cha wachezaji 20 kwenda Algeria ikipitia Misri, lakini hata hivyo kuumia kwa mabeki Juma Nyosso na Kelvin Yondan kwenye mechi ya leo dhidi ya African Lyon kunaiweka katika wakati mgumu klabu hiyo kuamua wachezaji wa kuwaacha kwa safari hiyo. Juma Jabu naye ni majeruhi hataenda Algeria.

Comments