SIMBA WAINGIA KAMBINI BAMBA BEACH


VINARA wa ligi kuu bara na wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye
michuano ya Kimataifa Simba, wameingia kambini leo kujiandaa na
michezo yake ligi hiyo na ile ya kimataifa.

Simba imengia kambini baada ya kushinda mechi yake ya kombe la
Shirikisho (CAF) jumapili iliyopita dhidi ya Es Setif ya Algeria kwa
mabao 2-0 katika mechi iliyopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es
Salaam.

Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema kikosi chote cha Simba
kimeingia kambini katika hoteli ya Bamba Beach iliyopo Kigamboni
jijini Dar es Salaam na itakuwa ikifanya maandalizi yake huko huko.

Alisema wachezaji wote wapo katika hali nzuri na ari ya kufanya vema
katika michezo yao ya hivi karibuni wakianza na ule wa ligi kuu bara
dhidi ya African Lyon jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa.

Comments