SIMBA NA TOTO PUMZI SAWA

SIMBA ya Dar es Salaam imelazimishwa sare 0-0 na Toto African ya Mwanza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii.
Kwa matokeo hayo, Simba inarejea kileleni mwa ligi hiyo kwa pointi zake 41, sawa na Azam lakini yenyewe ina bao moja zaidi na iko nyuma kwa mchezo mmoja.
Yanga, mabingwa watetezi waliofungwa 3-1 na Azam jana wako nafasi ya tatu. Mbio za ubingwa wa Ligi Kuu, sasa wazi ni wa farasi watatu, Simba, Azam na Yanga- maana yake ligi ya mwaka huu ina msisimko zaidi, kwani timu tatu zinawania nafasi mbili za kucheza michuano ya Afrika mwakani.


Comments

  1. Mmmmmmmmmmmh Dina mbona nimesikia kuwa ni 0-0 sasa hii 1-1 imetoka wapi?
    wako
    James

    ReplyDelete

Post a Comment