SIMBA, KIYOVU WACHANGA MILIONI 208


MECHI ya Kombe la Shirikisho Afrika, kati ya Simba SC na Kiyovu ya Rwanda imeingiza kiasi cha 208,843,000.00, imeelezwa.
Mechi hiyo iliyosimamiwa na kampuni ya Prime Time Promotions ya Dar es Salaam, ilichezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na SImba ilishinda mabao 2-1, yote yakitiwa kimiani na Felix Sunzu.
Simba imeingia Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2, kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza mjini Kigali.  
Hata hivyo, mapato hayo hayafui dafu kwa mapato ya mechi ya kwanza ya Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Zamalek ya Misiri, ambayo iliingiza Sh 286, 695.000,00 wiki tatu zilizopita kwenye Uwanja huo huo.
Katika mchezo, timu hizo zilitoka sare ya 1-1 Yanga ikitangulipa kupata bao lililofungwa na Hamisi Kiiza na Zamalek kusawzisha kupitia kwa Amr Zaki.

Comments