SIMBA IPO FITI 100%

SIMBA imeshangazwa na taarifa za kuwepo kwa majeruhi ndani ya kikosi hicho ambacho kinajiandaa na mchezo wake wa kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Es Setif ya Algeria utakaopigwa keshokutwa kwenye dimba la Taifa.
Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti leo kuwa wachezaji wake Mwinyi Kazimoto na Jonas wamejeruhiwa hivyo kuleta hofu kuelekea mchezo huo, lakini msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo na Watanznia kwa ujumla na kusema kuwa timu hiyo ipo fiti kwa asilimia 100.
"Tunashangazwa na taarifa hizi zinatojka wapi jamani, wachezaji wote wapo fiti isipokuwa JUma jabu tu na kila mtu anajua napenda kuwatoa hofu Watanzania na mashabiki wa Simba jkwa ujumla"Alisema Kamwaga.
Aidha, Kamwaga alisema timu hiyo leo imelazimika kujifua katika dimba la TCC Chang'ombe ili kupisha ukarabati mdogo kwenye uwanja wa Taifa na kesho timu hiyo pamoja na wapinzani wao Es Setif watafanya mazoezio katika dimba la Taifa.

Comments