SBL YASITISHA MKATABA WA KUIDHAMINI STARS


KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL), imesitisha udhamini wake kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ulioanza mwaka 2006 kufuatia kupandishiwa dau la kuidhamini timu hiyo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Habari za kiuchunguzi, ambazo ziomepatikana jijini Dar es Salaam  zimesema kwamba SBL iliyoanza kuidhamini Taifa Stars kwa dau la Sh. Milioni 700, imetakiwa na TFF kutoa Sh. Bilioni 3.6 kwa mwaka kuidhamini timu hiyo.
Ofisa mmoja wa TFF, ambaye hakutaka kutajwa jina aliiambia bongostaz jana kwamba pamoja na hayo mazungumzo bado yanaendelea baina ya SBL na shirikisho hilo'
Hata hivyo, Ofisa huyo wa TFF alisema shirikisho limeahidiwa udhamini mnono kutoka kampuni nyingine kubwa ya bia nchini.
"Lakini kwa kuzingatia pale ambapo SBL wameitoa Taifa Stars, waliichukua haina mdhamini na hakuna mtu au kampuni iliyokuwa tayari kuidhamini, wamefanya mambo mengi kwa manufaa ya soka hii, kwa kweli hata mimi ningependa SBL iendelee kudhamini timu hii,"alisema Ofisa huyo.
TFF iliipandishia dau la udhamini SBL kutoka Milioni 700 hadi 800, baadaye 900 na mwaka jana ilikuwa n Sh Bilioni 1.2.
TFF sasa inataka Sh Bilioni 3.6 kwa mwaka na kwa sababu mkataba wa udhamin baina ya pande hizo mbili uliisha tangu Desemba, Taifa Stars haina mdhamini kwa sasa.
Teddy Mapunda, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa SBL alipoulizwa kuhusu mustakabali wa u suala hilo, alikiri kwa sasa mambo yote yamesimama kwa sababu mazungumzo yanaendelea kati yao na TFF.

Comments