SASA NI ZAMU YA WAKAZI WA DAR KUAMBULISHWA MSANII MPYA WA MSONDO NGOMA


BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma inatarajia kutoa burudani  katika jiji la  Dar es Salaam kwa ajili ya kumtambulisha mwana mziki wao mpya Shabani Lendi.
Akizungumza Dar es Salaam Leo, Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema, baada ya kuwa Zanzibar na kutoa burudan kwa kumtambulisha Msanii huyo.Sasa imepanga kumtambulisha siku ya Alhamisi ambapo watakuwa Kilimani Pub, Stakishari,Ijumaa Lidaz Clab, Kinondoni, Jumamosi TCC Klabu na Jumapili watakuwa katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni kwa ajili ya kumtambulisha Kikamilifu msanii huyo.Super D amewataka wakazi wa Dar es Salaam na Mikoa ya Jirani kuhudhuria kushuhudia burudan hiyo watakayoitoa ikiwa ni pamoja kusikia nyimbo zao mpya ambazo ni miongoni mwa nyimbo zitakazo kuwa katika albamu yao mpya ya mwaka huu ikiwa ni pamoja kusikiliza nyimbo zao za zamani.

Alizitaja nyimbo hizo mpya kuwa ni Suluu ya Shabani Dede,Nadhiri ya Mapenzi ya Juma Katundu, Mjomba, Dawa ya deni kulipa na lipi jema ambapo albamu hiyo inatarajia hivi karibuni.

Comments