SAMSON MBEGA AAGA DUNIA


MWANDISHI mwandamizi wa habari za michezo nchini, Samson Mbega amefariki dunia asubuhi ya leo- kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa marehemu, Mawazo Lusonzo ni kwamba msiba upo nyumbani kwa marehemu, nyuma ya kota za Temeke mwisho eneo la Pile Bar.
Mbega alikuwa mpole, daima ni kaka ni kiongozi, hakuwa na makuu. Ni aina ya watu adimu na kifo chake ni pigo. Huo ni ukweli usiofichika. Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin. Endeelea kufuatilia mamapipiro kwa taarifa zaidi za msiba huo.

Comments