ROONEY AIPAISHA KILELENI MAN UNITED


Mshambuliaji wa Man United, Wayne Rooney akishangilia jioni ya leo, Uwanja wa Old Trafford, Manchester, England baada ya kuipiga West Brom Albion mabao 2-0.  Mabao ya Man United yalifungwa na Wayne Rooney dakika ya 35 na 71, la kwanza pande la Javier Hernandez na la pili pasi ya Ashley Young. United imefikisha pointi 67 baada ya kucheza mechi 28 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, baada ya Man City kupigwa 1-0 na Man City jioni leo.

Comments