POULSEN ANYWEA KWA SAMATTA

KELELE nyingi zilizoelekezwa kwa kocha mkuuu wa timu ya Taifa, Jan Poulsen kutokana na kumtosa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)  Mbwana Samatta, hatimaye zimezaa matunda.
Poulsen alimtema Samatta kwa madai ya kushuka kiwango hivi karibuni alipotangaza kikosi cha timu hiyo ambacho kiliingia kambini kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu fainali za Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbuji ambapo katika mchezo wao uliopigwa jumatano iliyopita walilazimisha sare ya bao 1-1.
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya wadau wa soka walimpinga Mdenmark huyo na kusema kwamba huo ni mtazamo wake binafsi kwani nyota huyo aliyewahi kukipiga Simba Sc kiwango chake kipo juu na anaifanyia mambo makubwa timu yake inayoshiriki ligi kuu ya huko.
Baada ya kelele hizo, Poulsen ameweka wazi dhamira yake ya kwenda DRC kumshuhudia mchezaji huyo katika baadhi ya michezo.

Comments