PINDA, NCHIMBI WAIFAGILIA SIMBA

WAZIRI mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dk.Emmanuel Nchimbi wameiopongeza timu ya soka ya Simba kwa kuweza kuifunga Es Setif ya Algeria katika mechi ya kombe la Shirikisho (CAF) iliyopigwa jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Taifa na Simba kushinda mabao 2-0.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi hao pamoja na kuipongeza Simba walisema ushindi huo ni faraja kwa mashabiki na wadau wa Simba kwa ujumla.
Hata hivyo waliitaka timu hiyo kutobweteka na ushindi huo na kufanya maandalizi mazuri ili kuweza kushinda katika mechi ya marudiano itakayopigwa ugenini wiki ijayo.

Comments