PIGO ARSENAL, ARTETA NJE LEO


KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kiungo Mikel Arteta atakosa mechi ya leo ya Ligi ya Mabingwa dhidi yan AC Milan.
Mchezaji huyo wa zamani wa Everton aliuamia kichwani kwenye mechi dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield, ambayo timu yake ilishinda 2-1 mwishoni mwa wiki baada ya kugongana na Jordan Henderson.
“Tumewapoteza Benayoun, Diaby na Arteta naye. Arteta anatakiwa kupumzika kwa wiki moja. Rosicky yuko katika hatihati pia. Lakini tutashusha kikosi kizuri ili kufuzu,”alisema Wenger.
Kocha wa The Gunners anajiamini kikosi chake kinaweza kufuzu licha ya kutakiwa kufunga mabao manne.
“Tunaweza kufunga mabao. Katika mechi mbili zilizopita za nyumbani tumefunga mabao 12. Lazima tujenge uwiano sawa katika kushambulia na kuzuia.
“Kama Milan inaweza kufunga nne, tunaweza kufanya hivyo pia … tunajua tunaweza kuonyesha kiwango kizuri.”
Mfaransa bado anaamini timu yake inaweza kuwakatamata Tottenham katika Ligi Kuu licha ya wapinzani wao kuwa mbele kwa pointi nne, zikiwa zimebaki mechi 11.
Pia anahisi timu yake haina cha kupoteza ikicheza na Milan leo, lakini amekiri wanatakiwa kujitoa kwa kila kitu dhidi ya wapinzani wao hao kwenye Uwanja wa Emirates.
“Nilisema, si jambo lisilowezekana [kuwakamata Tottenham] kwa sababu tulitakiwa kucheza nao… tumekuwa mwendelezo,”alisema Wnger.

Comments