PETER MSECHU AFUTA MPANGO WA KUTOA ALBAM


MMOJA ya washindi wa shindano la muziki la Tusker All Stars 2011,  Mtanzania Peter Msechu  amesema licha ya kazi zake kupokelewa vema na mashabiki, hana mpango wa kutoa albamu.
Msechu ambaye kwa sasa anatamba na singo yake ya Relax aliyomshirikisha Kidum amesema kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na unyonyaji wa kazi za wasanii unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara. 
Alisema wasanii wengi wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika kutayarisha albamu zao lakini mwisho wa siku zinapoingia sokoni wanajikuta wakipata hasara huku wafanyabiashara hao wakifaidika.

Comments