PAPIC AVUNJA MAZOEZI YANGA

KOCHA mkuu wa Yanga Mserbia Kostadin Papic juzi alivunja mazoezi ghafla kutokana na kuchukizwa na wachezaji wake kumuwekea ngumu kipindi cha kuanza mazoezi.
Hali hiyo ilitokea katika uwanja wa Tipper Kigamboni ambapo Yanga ilikuwa inafanya mazoezi ya kujiansdaaa na mchezo wake wa ligi kuu bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga utakaopigwa jumamosi katika dimba la Mkwawani,Tanga.
Papic alipandwa na hasira hizo baada ya wachezaji kuendelea kufanya mazoezi binafsi licha ya kuwaita hivyo kuona kama ni utovu wa nidhamu.
Baada ya kufanikiwa kuwaita na wachezaji hao kujikusanya Mserbia huyo alitangaza kuvunja mazoezi na hivyo kuacha kila moja akibaki na maswali kichwani.

Comments