OKWI, KIIZA WATEMWA UGANDA CRANES, NDORO NDANI



NYOTA wa Uganda wanaokipiga Tanzania Emmanuel Okwi (Simba) na Hamis Kiiza wametemwa katika kikosi cha taifa cha nchi hiyo 'Uganda Cranes' ambacho jumamosi kitacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Misri huko Khartoum, Sudan.
Kwa mujibu wa taarifa toka vyombo vya habari nchini Uganda, kocha mkuu wa Ceanes Bob Williamson ameita nyota 22 huku akimuita kundini kinda linalokipiga katika klabu ya Yanga, Tonny Ndoro.
Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi kwa timu hizo katika kampeni ya kuwania tiketi za Kombe la Dunia 2014 na Kombe la Mataifa Afrika 2013.
Williamson amewaita katika kikosi hicho pia makinda Derrick Fabian Kizito ambaye anayecheza soka nchini Uholanzi, na Ronny Martins Lwanyaga anasakata gozi katika klabu ya  El Merrikh ya Sudan.
Wengine ni Mike Mutyaba anayechezea El Merrikh, beki Denis Guma wa  Victoria University na  Steven Bengo kutoka SC Villa.
Kikosi kamili: Ali Kimera, Hamza Muwonge, Denis Guma, Godfrey Walusimbi, Robert Kimuli, Edgar Luzige, Steven Bengo, Noah Ssemakula na Israel Emuge.
Saaka Mpima, Caesar Sapeo, Kizito Luwagga, Isaac Kirabira, Saddam Juma, Fabian Kizito, Ronnie Lwanyaga, Tonny Ndoro, Nicholas Wadada, Jimmy Kakembo na
Mike Mutyaba.

Comments