NITAVAA VIATU VYA MWAMEJA J'2-KASEJA

KIPA namba moja Tanzania Juma K Juma amesema kuwa atafanyia kazi ushauri aliopewa na kipa wa zamani wa timu hiyo Mohammed Mwameja ili kuweza kuwatoa nishai wapinzania wao kwenye kombe la Shirikisho ES Setif ya Algeria.
Kaseja anayeidakia Simba anatarajiwa kuwaongoza wenzake katika mchezo huo utakaopigwa jumapili hii kwenye dimba la Taifa.
Akizungumzia mchezo huo, Kaseja alisema pamoja na maandalizi mazuri wanayoendelea kuyafanya kuelekea mchezo huo, atatumia vema ushauri aliopewa na 'kaka' zake wakiwemo Mwameja ambaye aliwahi kuingoza timu hiyo kuitoa timu ya Algeria katika mashindano hayo miaka ya nyuma.
Mwameja ambaye baada ya kustaafu kuichezea Simba alimwachia mikoba Kaseja, amemtaka kipa huyo kufanya maamuzi magumu ili ambayo anaamini yataiwezesha Simba kushinda mchezo huo.

Comments