NG'OMBE HAZEEKI MAINI:YANGA SC

MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Yanga wametamba kuionyesha ukongwe wao wa Ligi hiyo Azam Fc ambayo kesho watakutana kwenye mchezo wa ligi hiyo utakaopigwa katika dimba la Taifa, jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu amesema kuwa kikosi chao kipo vizuri kwa mchezo huo ingawa utakuwa na upinzani mkubwa kutokana na ubora walionao Azam lakini na ushindi kwao muhimu.
“Kila mtu nafahamu ubora wa Azam lakini hilo halitutii hofu ya kuona tumeshafungwa kwani ng’ombe hazeeki maini, tunaiheshimu sana Azam lakini  dakika 90 ndizo zitaamua nani zaidi,”Alisema  Sendeu.
Sendeu aliongeza kuwa wachezaji wa timu hiyo wapo katika hali nzuri na tayari kwa mchezo huo isipokuwa Salum Telela na kipa Yaw Berko waliokuwa majeruhi kwa sasa hali zao zimetengemaa na wameanza mazoezi mepesi.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHMarch 10, 2012 at 7:36 AM

    HIVI MWANANGU HUWA MNAWAOGOPA SANA HAWA WATOTO WA MWANZA EEEEH?

    KWELI LAKINI MAANA WANAWATIAGA ADABU KWA MIGOLI MINGI MINGI.


    MDAU WA BOMBA LA UHURU,REVERE,MASACHUSETTS,USA

    ReplyDelete

Post a Comment