VIONGOZI SIMBA WAJARIBU KUZIMA MGOMO LAKINI BADO HAKIJAELEWEKA


Na Dina Ismail
PAMOJA na uongozi wa klabu ya soka Simba kukanusha kwa nguvu zote kuwepo kwa mgomo wa wachezaji, ukweli ni kwamba kuna mgomo wa chini chini unaendelea ndani ya timu hiyo.
Habari za ndani za klabu hiyo zinaeleza kwamba licha ya kambi kuanza juzi katika hoteli ya Bamba Beach iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam kuna baadhi ya wachezaji hawakuripoti kwa sababu tofauti lakini ukweli ni kuwa wanashinikiza kulipwa fedha zao. 
Taarifa zinaeleza kuwa uongozi uliahidi kuwapa kiasi cha shilingi mil.30 kama wangeshinda mechi yao yao ya kwanza ya kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Es Setif ya Algeria jumapili iliyopita na ambapo Simba ilishinda mabao 2-0.
Hata hivyo uongozi uliwapatia wachezaji hao shilingi milioni 15 tu tena ambazo zinadaiwa kutolewa na mmoja ya wadau wa timu hiyo Azim Dewji kama motisha ya wachezaji hao kuifunga Es Setif, hali ambayo haikuwapendeza wachezaji wa timu hiyo na kuamua kuendesha mgomo.
Imedaiwa kuwa kuna baadhi ya wachezaji wameripoti kambini lakini mgomo unaendelea chinichini huku wakiapa kutojitum akatika mechi yaop ya ligi kuu dhidi ya African Lyon mwishoni mwa wiki kabla ya kufanya hivyo katika mchezo wa marudiano dhidi ya Es Setif wiki ijyo.
Akizungumzia hilo, ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alikanusha kuwepo kwa mgomo na kudai kuwa taarifa hizo zinaenezwa na watu wasioitakia mema klabu hiyo ambayo kwa sasa ipo imara. 
Alisema wachezaji ambao hawakuripoti kambini  jana kila mmoja alikuwa na sababu za msingi zilizomfanya asiripoti kambini ambapo wengi wao waliripoti jana.
“Kuna watu wanataka kutuvuruga katika kipindi hichi ambacho Simba ipo makini zaidi katika mashindano muhimu….suala la wachezaji kudai posho za mchezo halina ukweli wowote kwani walishalipwa kinachostahili,”alisema Kamwaga. 
Kamwaga aliongeza kuwa  mkataba wa Simba hauelezi kuwa mchezaji anatakiwa kulipwa kwa mechi za kimataifa hivyo hata fedha walizowapa ilikuwa ni sehemu tu ya kuwatunuku kutokan na kujituma kwao lakini hazimo ndani ya mkataba.






Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHMarch 28, 2012 at 6:55 PM

    FRIENDS OF SIMBA HUWA HAWAPENDI MAFANIKIO YA SIMBA AMBAYO WAO HAWAJASHIRIKI KUYALETA,ALWAYS WANAPENDAGA WAONEKANE WAO NDIO WAO NA BILA WAO HAKUNA MAFANIKIO SIMBA,HIVYO YANAPOTOKEA MAFANIKO NDANI YA SIMBA AMBAYO HAYAKUWAHUSISHA WAO HUWA WANATAFUTA KILA MBINU KUIVURUGA TIMU KWA KUWATUMIA WAANDISHI WA HABARI NA WANACHAMA WANAOJIITA MAARUFU,NAWAPONGEZA SANA KINA ADEN KWA KUWADHIBITI ANGALAU SO FAR,YOTE NI KWA KUWA ADEN NI MTU WA MJINI,FRIENDS WENGI NI WA TU WA KUJA TU AMBAO WALIINGIZWA SIMBA NA MZEE WA TANDAMTI KARIAKOO NDUGU YANGU KD..!

    SAYZ MDAU WA BOMBA,REVERE,BOSTON,MASACHUSSETTS.

    ReplyDelete

Post a Comment