MWANAFUNZI wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya
St. Anthony Mbagala, mkoani Dar es
Salaam , Franco Donald Kisongo (18), amepotea jijini
humo.
Shangazi wa kijana huyo, Adelaide Kisongo amesema, Franco ni
mgeni jijini Dar es Salaam amepotea tangu Jumapili asubuhi ikiwa ni siku nne tu
tangu ajiunge na shule hiyo kuanza masomo ya kidato cha tano.
Kwa mujibu wa Adelaide ,
kijana huyo aliwaaga wanafunzi wenzake kuwa alikuwa anakwenda kwa shangazi yake
Kariakoo, hakufika huko, na pia hakurudi shule na hadi sasa haijulikani alipo.
Amesema, walimu na walezi wa kijana huyo Mrangi, wametoa
taarifa katika vituo vya Polisi Mbagala Kizuiani, Chang’ombe na Msimbazi, na
wanatumia RB namba 3343/2012 ya kituo cha Msimbazi kumtafuta.
Kwa yeyote mwenye taarifa kuhusu mahali alipo kijana huyo
anaombwa kutoa taarifa kituo chochote cha polisi au kuwasiliana na wenye namba
zifuatazo za simu. 0784- 384035,
0717-371763, 0713- 761006, na
0715- 247544
mwisho
Comments
Post a Comment