MUAMBA BADO HALI YAKE SI NJEMA


Muamba
BEKI wa Bolton, Fabrice Muamba bado yuko mahututi katika chumba cha wagonjwa walio chini ya uangalizi maalum baada ya kuzimia jana, imesema taarifa ya pamoja kati ya klabu yake na hospitali ya London Chest.
"Kama ilivyo ada ya zoezi la tiba, Fabrice bado yupo chini ya uangalizi maalum na atakuwa huko kwa angalau saa 24," ilisema taarifa hiyo. "Hali yake bado inatazamwa kwa karibu mno na wataalamu wa hospitali."
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, mzaliwa wa Kinshasa, DRC alikimbizwa hospitali baada ya kuanguka uwanjani na kupoteza fahamu mwishoni mwa kipindi cha kwanza katika Robo Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye Uwanja wa White Hart Lane jana.

Comments