MUAMBA ALIKUWA MFU KWA DAKIKA 78


Daktari wa timu ya Bolton Wonderers Jonathan Tobin ameelezwa kwamba nyota wa timu hiyo Fabrice  Muamba alikuwa mfu  kwa zaidi ya dakika 78, kutokana na ugonjwa wa  Moyo ambao ulisabababisha  lililomdondosha uwanjani mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kutokana na hali hiyo Muamba alikimbizwa katika hospitali ya  London Chest na kulazwa katika  chumba cha uangalizi maalum (ICU), huku madaktari wakisema ni mapema sana  kubaini kama nyota huyo ataweza kucheza tena soka.
Hata hivyo Dk. Tobin amesema kuwa marejeo ya fahamu aliyoyapata kiungo huyo mwenye miaka 23 yanamjaza matumaini ya kupona haraka. "Tulijawa hofu kubwa mno na hatukufikiria kwa wakati huo kwamba angerejea katika hali ya kawaida. Ilikuwa ni ajabu mno."
Muamba alipata janga la moyo dakika ya 40, wakati akiichezea Bolton mechi ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye uwanja wa White Hart Lane Jumamosi na kukimbizwa London Chest kwa matibabu zaidi.

Comments