MTU HAWI NA HATIA MPAKA ATAKAPOTIWA HATIANI-WAMBURA AJIBU MAPIGO



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: TAARIFA ILIYOTOLEWA NA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI WA
Nimepokea taarifa za shutuma mbali mbali dhidi yangu zilizotolewa na Bw Lyatu  kupitia kwenye magaazeti mbali kupitia kwenye mitandao pamoja na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Bw Lyato 6/3/2012, Awali ya yote ningependa watanzania wafahamu kuwa Kamati hiyo ya uchaguzi ya TFF haijawahi kuwa huru na haijawahi kufanya  maamuzi ya haki dhidi yangu hata mara moja, silazimishi wafanye hivyo ila katika kufuatilia haki kuna siku ukweli utajidhihiri, labda niwakumbushe, baada ya uchaguzi 2004 kuisha ambapo niligombea uraisi wa TFF  na ndugu L.Tenga ambapo tenga alishinda, baada ya hapo  mambo mengi juu yangu yalianza kujitokeza . Mwaka 2005 iliamuriwa ufanyike uchunguzi wa mahesabu (Auditing) tangu nilipoingia madarakani wakati huo FAT 2002,2003 na2004 kampuni iliyopewa kufanya ukaguzi  huwo ilitoa orodha ya watu na malipo mbalimbali ambayo hayakuambatana na hati za malipo zilizoidhinishwa “List of Un approved vouchers with no supporting Documents” ambazo kimsingi ni kama Hoja za kiukaguzi “Audit Querries” lakini haikuwa hivyo.
Tarehe 14/01/2006 TFF ilifanya mkutano wake mkuu wa kawaida wa mwaka 2005, katika mkutano huo yaliwasilishwa mahesabu ya fedha ambayo sio final Audited Accounts ambayo yalilenga kunidhalilisha na kunishushia heshima mbele ya jamii, wakati huo mimi nilikuwa mjumbe wa mkutano mkuu kupitia Klabu Simba kama mwenyekiti nilihoji utaratibu huo, taarifa hiyo ya fedha ilitolewa ndani ya ukumbi bila wahusika nikiwemo mimi kupewa hoja zinazonihusu na muda wa kujibu hoja hizo, Kwa kawaida mkutano mkuu hupelekewa Taarifa kamali ya mahesabu iliyokaguliwa(Audited Accounts) baada ya kupata majibu ya hoja za kiukaguzi kutoka kwa wanao husika jambo ambalo halikufanyika kwenye hili. Baada ya kulalamika miezi mitatu baadae Tarehe 21/4/2006 niliandikiwa Barua na TFF yenye kumbukumbu TFF/ACC.06/2 yenye kichwa cha habari “QUERIES ON PAYMENTS MADE TO YOU” yaani hoja zinazohusiana na malipo yaliyofanya kwako, aidha barua hii ilinitaka mimi nikiwa mmoja wa watu waliotajwa kwenye orodha ya watu waliolipwa malipo mbali mbali ambayo hayana viambatanisho hivyo  kupewa siku 30 kutoa maelezo na majibu stahilli ili kufanikisha ukaguzi Maalum (SPECIAL AUDIT) katika maenoa matatu(3): 
1.   Kutathmini malipo ambayo hayakuidhinishwa yaliyofanywa kwa viongozi wa FAT kamailivyo ainishwa kwenye pendekezo 12. 2.   Kuanisha uhalali wa madeni ya FAT mpaka 2004. 3.   Kutathmini uhalali wa gharama za vifaa (Fixed Asset) zilizonunuliwa 2002-2004. Tarehe 28/5/2006 niliandika maelezo na majibu yote ambayo nilitakiwa kuyatolea  maelezo, hoja zote zilizo letwa kwangu zilijibiwa, sikupata maelezo mengine yoyote au maswali ya kutaka ufafanuzi wa jambo lolote linalohusu ukaguzi.
Baada ya taarifa ya ukaguzi maalum kutoka niliipata kwa njia zangu na kuisoma nikagundua kuwa ukaguzi huo huenda ulinilenga mimi maana watu wote waliotoajwa kwenye ukaguzi wa awali hawakutajwa tena, taarifa haikusema kama majibu yao yalitosheleza matakwa yao na haikutaja kama majibu yangu hayakuwatosheleza na kukidhi mahitaji yao. Katika Taarifa ya ukaguzi Maalumu (Special Audit) Kifugu 4.0 (a) mkaguzi anasema viongozi wa FAT hawakuweza kupatikana kutoa maelezo kuhusiana na hoja za kiukaguzi, hii inamaanisha kuwa majibu ya hoja niliyoyawakilisha TFF tarehe 28/5/2006 hayakupelekwa kwa wakaguzi na kama mkaguzi alinihitaji basi TFF ilimweleza sipatikani, ili report ionekane mimi ni mbadhilifu.
Kifungu 4.0(b) cha taarifa hiyo pia kinasema kazi ya ukaguzi maalum imekuwa ngumu kwa kuwa viongozi wa FAT hawajakabidhi ofisi hivyo nyaraka zinazohusiana na ukaguzi huo kutokupatikana, hili ni jambo la kushangaza kwani nilkabidhi ofisi siku mbili baada ya uchaguzi 29/12/2004 na wakati ukaguzi huo unafanyika mwezi 7-8/2006 iliisha pita miaka 2 swali linakuja kazi za TFF zilikuwa zinafanyikaje? Mimi sikuwa mhasibu wa TFF ambaye nina tunza nyaraka za malipo, mhasibu wa TFF mpaka hivi sasa yupo walishindwa nini kumuuliza? Ninachokiona mimi hizi zilikuwa ni njama zilizofanywa kuficha nyaraka ili majibu yasipatikane ili nionekane mbadhilifu na mwizi. Kifungu4.0(e) cha ukaguzi kinasema wamegundua makosa mengi ya uandikaji wa kumbukumbu za mahesabu katika vitabu vya FAT, hiyo inamaanisha kumbukumbu walizopatiwa hazikuwa sahihi na hivyo zilipaswa kuwekwa sawa kwanza ili ukaguzi ufanyike jambo ambalo lilikuwa gumu kwa mkaguzi kwa kuwa nyaraka nyingi hazikuweza kupatikana Mfano PV 5322 ya tarehe 22/6/2004 inaonyesha malipo $ 3250 kwa ajili ya posho za safari kwenda Ruanda halafu maombi ya idhini ya malipo iliyoambatanishwa nayo inataja PV 5322 Mr Wambura malipo ya PTA’s for match kamisaa ya $350.
Ili nionekane mbadhilifu Nimegundua maombi mengi ya uongo na kutunga ya idhini ya malipo yameandikwa kuonyesha nilipokea malipo bila sahihi yangu ili mradi yaonekane yalifanyika kwangu mfano 28/07/04  PV 5324.
Pamoja na Mkaguzi katika repoti zake nyingi tangu ya awali kuitaka TFF iwasiliane na mimi ili majibu yapatikane TFF haikuwahi kufanya hivyo kwa makusudi na kwa hila na nia mbaya na mimi .
Mwaka 2008 niligombea nafasi ya Makamu wa pili wa rais wa TFF katika mchakato huo jina langu liliondolewa katika orodha ya wagombea, nilikata rufaa katika kamati ya Rufaa ya TFF, katika moja ya hoja za TFF ni kwamba kuna hoja za kiuhasibu ambazo sikuwa nimezijibu, hii ndio ilinionyesha ni kwa jinsi gani majibu yangu yalifichwa na mkaguzi hakupewa, kwani mjibu yale yalikuwa na nakala 3 na niliyakabidhi TFF 2006 iweje 2008 hawajayapata? , hivyo ikaamuliwa nipewe hizo hoja nizijibu. Tarehe 1/12/2008 TFF iliniandika barua nyingine yenye Kumbukumbu TFF/ADM/AP.08/07 yenye kichwa cha habari “YAH: HOJA ZA MAHESABU YA FAT (TFF)”  iliyosainiwa na Mtemi Ramadhani, katika barua hii tff ilinitaarfu kuwa kamati ya Rufaa iliyoketi tarehe 5/12/2008 imenitaka nijibu hoja za kiukaguzi kabla ya tarehe 10/12/2008 saa 6.00 mchana na ofisi itakuwa wazi kushirikiana na mimi kupata nyaraka hizo ili zijibiwe, Jitihada za kupata nyaraka kutoka TFF ziligonga mwaba hakuna aliyekuwa tarayari kutoa ushirikiano, 7/12/2008 nilimwandikia katibu mkuu wa TFF nikimueleza juu ya malalamiko yangu kutokupa ushirikiano kutoka katika ofisi yake, na kuomba nipatiwe nyaraka muhimu kabala ya tarehe 8/12/2008 saa sita(6.00) mchana pamoja na nyaraka zifuatazo: 1.Nakala ya Ukaguzi maalum(Special Audit Report) 2.Vivuli vya Nyaraka mbali zikiwemo receipt na hoja za kiukaguzi  wa mahesabu.
Tarehe 8/12/2008 TFF kupitia barua yake TFF/ADM/GC.08/105 ilinijibu ikinitaarifu kuwa ofisi yake itanikabidhi nyaraka mbali mbali zinazonihusu niende nizifuate, nilipozifuata kama barua katibu mkuu ilivyosema, sikupewa ushirikiano wowote na niliyemkuta offisini nd Mtemi Ramadhani alikataa kabisa kutoa ushirikano, niliiandukia TFF barua nyingine kuelezea kukosa ushirikiano, tarehe 9/12/2008 siku moja kabla ya deadline nilipigiwa simu niende kuchukua nyaraka, nilipewa vivuli vya profoma invoice, Accounts ledger na barua moja ya kutoka kwa Marehemu Charles Masanja.
Tarehe 10.12.2008  kampuni ya Uhasibu na Ukaguzi ya E.K Mengesho & Company ilitarifu TFF kwa niamba yangu wakabidhiwe vielelezo na  hoja hizo za kiukaguzi,  kampuni hiyo kupitia barua yake Kumb MACO/AQR-MRW/12/08 iliitaka tff iwakabidhi nyaraka zifuatazo ili zijibiewe:
1.   Copy of complet the complete Special Audit Report 2.   Copy of all relevant documents touching Mr Wambura namely,2.1 Payment vouchers, 2.2 Invoices ,2.3 Receipts ,2.4 Personal Ledger,2.5 Journal Vouchers.
  Barua hiyo haikujibiwa hadi hii leo, aidha nilichukua jitihada za ziada kuwasiliana na wanasheria wa kampuni ya Uwakili  MSK LAW PARTNERS(ADVOCATES) nao waliwaandika TFF barua yenye kumbukumbu MSK/TFF/08/01 yenye kichwa cha habari MICHAEL. R. WAMBURA –Audit Queries kuwasisitiza TFF iliwaweze kunikabidhi nyaraka hizo bila mafanikio, hata hivyo barua zote mbili hazikujibiwa hadi hii leo.  Pamoja na vikwazo vingi vya kupata nyaraka kutoka TFF nilioomba kamati ya rufaa ikubali kupokea majibu ya hoja za kiuhasibu niliyoyatoa mwaka 2006 ili yaweze kuongoza kikao, aidha kamati hiyo ilikubali na kupitia hoja mbalimbali na kuridhika kuwa sikuwa na hatia ya ubadhilifu kama pingamizi lilivyowasilishwa, aidha sababu ya kuondoa jina langu ni waswasi na suala la Uadilifu (Intergrity) wa kuwa kampuni MIN INVESTMENT PROMOTION CO iliyofanya biashara na TFF ilikuwa inamilikiwa na Mimi Michael Wambura, ukweli ni kwamba kampuni hii inamilikiwa nd Josea Samuel kama inavyoonyesha katika Extract From Register No 93017 ya Msajili wa Makampuni, Mnamo tarehe 10/12/2008 Bw Josea aliiandika TFF barua akiambatanisha na vivuli vya Cheti cha Usajili akiitarifu TFF kuwa yeye ndie mmiliki halali wa Kampuni hiyo na ni yeye ndiye aliefanya biashara na TFF na kama kuna maelezo ya ziada yuko tayari kufiki pindi wakimhitaji, Kwa kuwa TFF walikuwa na agenda ya Siri juu yangu waliamua kuificha kamati ya rufaa juu ya taarifa(barua)hiyo  na hatimaye kamati ya rufaa kuondoa jina langu kwenye uchaguzi huo kwa sababu ambazo sio za kiubadhilifu.
Katika kuhakikisha majibu yanapatikana na kuweka wazi juu ya suala hili, na kama TFF inanituhumu kwa ubadhilifu ni kwanini nitumie nguvu zote hizo kupata nyaraka ili nipate kujibu hoja zao? Kulikuwa na sababu gani niwaandikie TFF barua 3 na nyingine kutoka kwenye makampuni ya ukaguzi na hata kutoka kwa wnasheria nabado walishindwa kunikabidhi hizo nyaraka hizo hata kujibu barua? Ununuzi wa Samani za Hostel Mwaka 1998 Fifa kupitia mradi wa FIFA Goal project iliipitisha Tanzania kuwa moja ya nchi wanachama wa Fifa ambao wangepatiwa mradi wa mendeleo katika awamu ya kwanza, Msimamizi Mshauri(consultant) MD Consultancy-architect aliteuliwa kusimamia mradi huu, mpaka 29/12/2001 uongozi mpya unaingia madarakani ujenzi mradi huu uliukuwa haujaanza kutekelezwa, aidha sababu zilizoleteleza ucheleweshaji pamaoja na nyingine ilikuwa,
1.   Kuwasilishwa kwa mapendekezo ya kubadili mchoro uliokuwa tayari umeidhinishwa na fifa kutoka Hostel ili ujengwe uwanja wa mpira (Stadium) 
2.   Kuchelewa kupatikana kwa vibali pamoja na hati mbali mbali zinazoonyesha manispaa husika iliridhia ujenzi huo,
3.   Kujua mmiliki halali wa karume Staduim
4.   Makandarasi kuandika maakadirio ya ujenzi kwa kutumia TSHs badala ya UDS($) Mwaka 2002 tulianza kusimamia ili kuhakikisha mradi huo unaaza kwani baadhi ya nchi zilikuwa zimeisha kamilisha awamu ya kwanza na kuanza kuitumia. Wakati mradi huo unaidhinishwa na FIFa, viwango vya kubadilisha fedha (Exchange Rate) itakuwa ni sh 436 kwa dola mpaka mradi utakapo kamilika ili kuondoa uwezekano wa mradi kushindwa kuendelea. Mwaka 2004 wakati mradi unakaribia kufika tamati ilioneka kuwa gharama za mradi ziliongezeka  na FAT haikuwa na uwezo wa kulipia, tarehe 7/7/2004, Fifa ilihamisha kiasi cha Dola $71,590.00 kutoka kwenye Accounti yetu ya FAP(Financial Assistance Programme) na kuifanya akaunti hiyo kubaki salio sufuri, uamuzi kama huo ulifanywa na fifa na mwanachama alikuwa anataarifiwa kwa kuwa malipo yalifanywa na wao moja kwa moja. June 2004 mradi ulikuwa umefikia hatua za mwisho kukamilika lakini katika BOQ(bills of Quantity) haikujumlisha Vifaa vya Hostel Pamoja na ukuta wa kuzunguka eneo lote la karume,na kwa kuwa jambo hilo halikuwemo kwenye mradi mshauri ujenzi alishauri zitafutwe hela kwa kuwa mradi huo ni mwingine tofauti na wa awali. Msimamizi wa Maendeleo wa kanda yetu nd Ashford Mamelodi alipokuja alikuta na kusema haiwezekani mradi ukazinduliwa katika hali hiyo,hivyo aliagiza yatafutwe makampuni yanayoweza kufanya  kazi  na yeye atashawishi fifa igharamie kazi hizi
1. Kujenga uzio(ukuta)
2. Kusupply furnitures za hostel Makampuni mengi yalikuwa hayapendi kufanya kazi na FAT/TFF kwa kuzingatia rekodi zake za fedha na ulipaji wake wa madeni, Makampuni machache yaliweza kukubali kufanya biashara na FAT tena kwa gharama kubwa kufidia muda na hasara nyinginezo ambazo wangeweza kukutana nazo ,makampuni kadhaa na yalileta Makisio ya gharama zao.Tulizipeleka FIFA, Nd Mamelodi alipokuja alikutana na wawakilishi wa makampuni hayo na alikubali kuwa atawalipa moja kwa moja. Mjenzi wa ukuta alilipwa moja kwa moja baada ya kumaliza kazi na kuikagua Malipo ya zabuni ya vifaa vya hostel yaliletwa FAT kwa kuwa sehemu ya fedha tulizoomba zingetusaidia kuiweka kambini  na kuisafirisha Serengeti Boys na twiga Stars kwenda Zimbabwe na Kigali. Lilikuja wazo la kununua Basi ili leweze kusaidia timu zetu za Serengeti na Twiga kusafiri mara kwa mara kwa kuwa basi lilokuwepo la FAT lilikamatwa na kupigwa mnada kutokana na madeni ya FAT ya mwaka 2000-2001, hivyo tulikubaliana katika $ 25,000/ zilizokuwa zimekuja tutoe Usd 10,000.00 ili kufanya malipo ya awali ya kununua Basi, kwa kuwa Fedha hizo zinatoka FIFA ilikuwa lazima Mwenyekiti wa FAT aidhinishe kwanza ndio hatua nyingine ifanyike kama inavyoonekana kwenye PV 5324 ya tarehe 29/7/2004 na barua ya mwenyekiti kwa wakaguzi, mpango wa kununua basi ulishindikana kwa kuwa FIFA iliagiza mzabuni alipwe pasipo maelezo mengine hivyo salio lililobaki la USd 8,400.00 lisingeweza kununua basi hivyo zilihamishiwa kwenye matumizi ya maandalizi ya  timu ya Serengeti Boys kwenda Ruanda kwa basi la kukodi na posho na Twiga stars kucheza na Zimbabwe ikiwa ni usafiri na posho zao, kumbukumbu za malipo na matumiz yako kwa mhasibu.
Kwa mujibu wa katiba ya FAT ibara 42(3) (e)&(k) katibu mkuu ndiye Afisa mhasibuwa chama (Accounting Officer)  na atabuni njia mbalimbali za kuongeza mapato ya FAT hivyo mamlaka yalikuwa yaniniruhusu kufanya na kuhamisha mafungu ya fedha(Realocation of Funds) kutoka katika kifungu cha matumizi ya  kununua basi na kupeleka katika matumizi ya timu za Taifa.
Tuhuma zote alizozitoa Nd Lyato kuhusu ubadhilifu  zilitolewa pia, lakini kamati ya rufaa chini ya JAJI Mkwawa  ili iliona sikua na hatia nazo na ushahidi wake unaweza kupatikana katika kumbukumbu za majadiliano (Proccedings),pamaoja na maamuzi yaliyotolewa hayakuwahi kunitaja mimi kuwa mbadhilifu au mwizi , hata kamati ya Uchaguzi chini ya Ng Lyato katika chaguzi 2 ambazo ni za Simba na Mara (FAM) katika barua zake haikuwahi kutaja kuwa jina langu linaondolewa kutokana na Ubadhilifu jambo linaloonyesha kuwa maneno aliyo yasema Lyato kwa waandishi wa habari ni yake binafsi na sio ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF. 
 Ninapenda kumfahamisha bwana Lyatu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema “ mtu hawi na hatia mpaka atakapo tiwa hatiani na Mahakama” hivyo kuendelea kunizuia kugombea kwa mambo ya kufikirika na ya kizushi ni kinyume na sheria jambo ambalo huenda likahitaji mkono wa mahakama kutafsiri ,
Bwana lyatu alijua mimi  ni mbadhilifu ni vipi nilipogombea uongozi wa FAM(Mara) alisahau kutumia kigezo hicho kwani sababu pekee iliyotolewa na kamati yake ilikuwaa ni mimi kuipeleka Simba Mahakamani, lakini hata kama ni kosa adhabu yake ni nini na imetajwa kwenye kifungu kipi cha kanuni na Katiba ya TFF?  Ni wazi bwana lyatu amejazwa jazba na upepo hata kutumia maneno ambayo kwa mtu anayefikiri kwa kutumia ubongo asingeweza kuyaandika ni wazi bwana Lyatu ameingia kwenye siasa za Uchaguzi wa TFF 2012,hivi sasa imegundulika kuna binadamu wawili (ufaransa na Uingereza) wamezaliwa na wanaishi bila ya kuwa na ubongo. Napenda kumhakikishia bana Lyatu umri wa kugombea uongozi TFF ni miaka 18 ambayo mimi niliisha ipita na hata kama ningechaguliwa leo ukomo wa uongozi wa TFF ni miaka 70 kwa mantiki hiyo sina sababu ya kudanganya umri,mimi nimezaliwa hospitali hivyo nina cheti cha kuzaliwa, nina passport, kadi ya kupigia kura nimesoma shule kuanzia Msingi, sekondari na Chuo kikuu DSM(UDSM) ambapo kumbukumbu zangu zote za kuzaliwa zinapatikana, kwa kuwa nakala za form hizo sijaziona siwezi kukubali au kukataa tofauti iliyojitokeza na kama ipo itakuwa ni kosa la bahati mbaya amboyo sikuidhamiria lakini pia nitapenda nione nakala halisi, mtu anayedanganya umri ni Yule ambae atakaefaidika kwa kufanya udanganyifu huo, iwapo sifa za kikatiba ni miaka 18 na mimi sina nikajaza hivyo hiyo itakuwa udanganyifu lakini kama nimeipita na nikaandika tofauti na bado ninakidhi matakwa ya kikatiba hapo nitakuwa sikudanganya umri bali nimekosea kujaza umri wangu mtu anayedanganya kama ambavyo nilikuandikia kuwa Katika wilaya za Temeke Kinondoni na Ilala kuna viongozi waliochaguliwa hawana elimu ya kidato cha Nne kama kanununi za TFF unazodai anazisimamia zinavyosema na huku akiendelea kuwa bubu na kiziwi huku sauti na masikio kufunguka suala linapokuwa linapomuhusu Wambura, Kwa kuwa hakuwa na nia njema na mimi, hata kanuni ndogo ya haki za binadamu ya haki ya mtu kusikilizwa(right to be heard) aliipuuza, kwani angeniuliza kuhusu utata huo angepata hasara gani? au angalichelewa kuongea na waandishi? .  Napenda kumkumbusha Lyato niliwahi kusema hawezi na hata kaa hata siku moja kunitendea haki, kwa mantiki hiyo nisingeweza kudanganya umri , ninachopenda ieleleweke ni vizuri kazi za watu zikabaki ofisini na mambo ya kijamii na kibinafsi (social and personal issues) zikabaki mitaani kwani unaweza kumfikira mtu na kumhukumu mtu kwa asilo litenda, kila wakati haki si tu itendeke lakini ionekana kutendeka “justice must not only be done must seen to be done’’ lazima maamuzi yafanyike posipokutilia chembe ya shaka.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF bila kuheshimu kamati ya Rufaa ya TFF imeanza kuandikia mikoa wanachama wa TFF kupinga maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya TFF yote hani kisa maamuzi yale yalimsaidia  Wambura na kwa kuwa mwaka huu kuna uchaguzi mkuu wa TFF, aidha kamati hiyo imeamua kunyakua madaraka ya kuwa msemaji wa TFF bila kujali athari za kisheria zinazoweza kuikumba tff kutokana matamshi na maamuzi ya kamati hii, ni wazi kamati hii inanyakua mamlaka ya kikatiba ya usemaji ya Rais na Katibu wa TFF, Humu duniani kuna aina nyingi za walevi wengine pombe wengine madaraka na wengine huwa mbumbumbu wa sheria na mambo mengine  lakini hawataki waelimishiwe, Mwl Nyerere alisema ni bora ukawa mjinga kulikoni mpumbavu maana mjinga anafundishika, hivi upeo wa bwana Lyatu kuelewa kuwa Kamati ya Rufaa ni supreme Organ(ni chombo cha cheye mamlaka ya juu) ndani ya TFF umeishia hapo? Ni kweli wafanyakazi wanatakiwa kupelekwa kozi mara kwa mara lakini kwa TFF kumpeleka Lyato kwenye hili itakuwa Ufisadi, hivi lyatu na kamati yake wanajua na kufahamu Sheria kulikoni Prof Mgongo Fimbo? Wanaufahamu wa masuala ya utawala wa michezo kuliko KIPINGU, TANDAU, Mhe MISANGA na  Kamanda RWAMBOW,? Nikisema huu ni ulevi sitakuwa nimekosea, ninachomshauri Nd Lyatu awaombe radhi watu hawa na ajiuzulu kwani yeye amekuwa mzigo mkubwa na kusababisha majeraha na madonda makubwa katika mpira wa Tanzania, kwani TFF na wadau wote hawazungumzii tena mpira bali uchaguzi za TFF.
Kuhusu swala la kwenda CAS napenda nimkumbushe bwana Lyato kwa kuwa yeye ni mbumbumbu wa sheria (ignorant in Law) maamuzi yakiisha fanywa na chombo cha juu yanakuwa Binding to the parties(yanafunga pande zote) ila  yule ambaye anadhani hakuridhishwa nayo ndie anayepaswa kukata rufaa kwa chombo cha juu zaidi, maamuzi ya Kamati ya rufaa yalikuwa upande wangu(in my Favour) hivyo siwezi kukata rufaa CAS ila kwa kuwa wewe hukuridhika namshauri uende huko ili upate haki unayoitafuta na kwa kuwa hakuna chombo cha juu kilichotoa uamuzi tofauti, maamuzi yanabakia valid mpaka hapo yatakapo tenguliwa, ni jambo la ajabu uamuzi uliotenguliwa ni wa kamati yake halafu anatangaza kutokutambua, njia nzuri ya kupinga maamuzi ni kukata rufaa sio kutotambua na kuifanya kamati ya rufaa kichekesho kwa kuandika barua mikoani nakuikashifu.
Kwa mujibu wa mtiririko wa vyombo vya haki katika katiba ya TFF inaanza Kamati ya Nidhamu,kamati ya Rufaa na Mahakama ya usuluhishi ya Michezo, Kanuni zinaundwa ili kurahisisha utekelezaji wa katiba hivyo kanuni haiwezi kuipinga katiba, Katiba ya TFF inasema Maamuzi ya kamati ya Rufaa ni ya mwisho na hayatajadiliwa na chombo kingine chochote isipokuwa CAS, wakati mamlaka ya kamati ya uchaguzi kuwa mwisho sio ya kikatiba ni ya kikanuni ambayo yanatungwa na Kamati ya utendaji ya TFF ila katiba inatungwa na kupitishwa na mkutano mkuu hivyo kwa Bw lyato kuipinga maamuzi kamati ya rufaa  hii inaonyesha ni jinsi gani mawazo yake  yamekosa nuru na yamefubaa  kutokana na upofu wa fikra sababu tu ya kujaribu kulinda maslahi yake na ya wenzake ili kiongozi wanayemtaka  aweze kuchaguliwa ili waendelee kuwa na nafasi ya kulivuruga soka la Tanzania. 
Bwana lyatu alikuwa mwenyekiti kamati ya kuchunguza mazingira na sababu zilizopelekea Serengeti Boys 2005 kuondolewa mashindanoni kama alijua kuna CAS na Tanzania ilikuwa na uewzo wa kushinda rufaa kama walivyo kata CAF ni kwanini aliacha nafasi ya Tanzania ikapotea bure na Tanzania kifungiwa miaka 2, ili hali anajua pahali kwa  kukatia rufaa ? hiyo ilitosha yeye na kundi lake kujiondoa TFF kwani kwa Tanzania kufungiwa mashindano ya U17 kumeliumiza sana soka la Tanzania 
Haikuwa nia yangu kutoa maelezo yote haya ila nadhani wakati mwingine mototo akipaliwa ukimgonga ngongoni maisha yanaanza upya kwa gharama nafuu, hivyo nimesema haya labda bwana Lyatu na kundi lake watapata ufahamu bila TFF kutumia fedha kwa ajili ya semina, ninapenda kusisitiza ni “kheri kuwa mjinga kuliko mpumbavu”(Nyerere J.K).
Ninapenda kusisitiza  kwakuwa tuhuma za bwana Lyatu zinazotokana na hoja za kiuhasibu(Audit Queries)  ambazo zote ni za uongo zenye nia ya kunifanya nipoteze hadhi mbele ya jamii aidha napenda kumhakikishia Nd lyato hili halitaniziba mdomo tutaendelea hadi wababaishaji mtakapo rudi mlipotoka, aidha ninapenda kumhakikishia  bw lyatu  katika uchaguzi 2012 utakapotangazwa nitachukua form na kugombea  katika nafasi nitakayo iona ni mwafaka kwangu bila kujali hila ghilba na fitna anazoniwekea, aidha kama yeye anavyodai  ni muadilifu ni vizuri kutumia fursa hii aliyopendelewa kushughulikia Suala la wilaya za DSM kwani kuna fununu kuwa amepewa au amepokea zawadi/ahadi ili suala hili lipite katika mazingira ya upendeleo kwani baadhi ya viongozi wa TFF ni  maswahiba na ni washiriki wa kambi moja ya uchaguzi ya TFF.
Ninamtaka bwana lyato awaombe msamaha watu wa Mara kwa udhalimu wa kuingilia mchakato wa uchaguzi huku akishindwa kuweka wazi mgongano wa kimaslahi na baadhi ya wagombe jambo linalopelekea kutilia shaka uadilifu wake. Ninapenda pia kuwapongeza wana CCM wenzangu  wa jimbo la ukerewe walioona ndugu lyato hafai kuwa mbunge wao kwa kumyima kura 2010 , kwani kuwanyima kura watu wenye uwezo kama balozi Kamanda, Mhe Mongela, na kumchagua kiongozi kama lyatu ingekuwa ni hasara ambayo wana ukerewe na taifa kwa ujumla tungejutia kwa muda mrefu kama kwenye mpira tunavyojuta. Mwaka 2008 ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa TFF ambapo tangia mwaka 2007 maandalizi ya wagombea yalianza mimi ni likuwa ni mmoja wa watu waliotangaza azma yangu ya kugombea tena katika uchaguzi mkuu wa TFF. Mwaka huo huo 2007 nilioonyesha nia ya kugombea tarehe 21/12/2007 TFF ilifungua jarada la malalamiko  kumb CD/IR/5110/2007 kwa Jeshi la Polisi kuwa kati ya 2002-2004 kulitokea ubadhilifu katika  ofisi za FAT  na mimi Michael Wambura nikiwa mtumishi wa FAT/TFF, Uchunguzi na upelelezi ulifanyika pamoja na kukusanya vielelezo na maelezo ya mashahidi mbali mbali na jeshi la polisi , hatimae jalada lilipelekwa kwa Mwanasheria mkuu wa serekali mwenye mamlaka ya kupitia na kusoma kuona kama kuna kesi ya kujibu dhidi ya mtuhumiwa . Tarehe 26/10/2011 jeshi la polisi kupitia barua kumbu DSM/ILAL/CD/B.I/I/VOL.XI/50 iliyosainiwa na Mkuu wa upelelezi makosa ya jinai Mkoa wa Ilala nd D. Nyanda-SSP ikiwataarifu TFF juu ya matokeo ya uchunguzi wao na maelekezo ya mwanasheria mkuu wa serekali ya barua kumb J/DSM/ILA/113/11 ya tarehe 1/4/2011 kama ifuatavyo
“Baada ya mwanasheria wa serekali kulisoma jalada hili aliridhika kuwa mtuhumiwa MICHAEL WAMBURA hakuwa na kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma hizo, Barua ya mwanasheria wa serikali Yenye kumbukumbu J/DSM/ILA/113/11  ya tarehe 1/4/2011 yahusika,  Kwa barua hii jalada la kesi limefungwa”
Kwa kuzingatia mlolongo mzima na mchakato mzima wa ukaguzi wa mahesabu ya TFF pamaoja na vikwazo vingi mbali mbali kutoka TFF tangu 2005 hadi 2012(miaka 8) ambavyo kimsingi vililenga kunichafua na kuniharibia jina ili nisiweze kugombea uongozi  na hatimae kuonekana mhalifu mbele ya jamii ni wazi vilifanywa kwa malengo Fulani ya watu Fulani kwa hila. Matokeo ya kamati ya Rufaa ya TFF mwaka 2008 hayakuniona mie mbadhilifu au mwizi, matokeo ya uchunguzi wa polisi na maelekezo ya mwanasheria mkuu wa Serekali yanatoa picha kamili ya Usafi wangu katika utendaji ambao kundi Fulani kwa maslahi yao wanajaribu kunifanya nionekane sifai, swali ninalojiuliza ilikuaje wakapeleka malalamiko polisi ya ubadilifu mwezi wa Dec 2007 na mimi kupewe hoja za kiuhasibu kujibu Dec 2008? Mwaka mmoja baadae, ni wazi kesi hiyo ilifunguliwa kwa hila na kwa manufaa ya watu Fulani.
nipenda watu wafahamu wakati mwingine haki haipatikani kwa urahisi ni lazima uipiganie sio tu kwa ajili yako ila pia kwa ajili ya watu wengine wanao weza kudhulumiwa haki yao Ninamtaka ndugu lyato nani ya Siku saba(7) aniombe radhi kwa maneno aliyoyasema juu yangu kupitia utaratibu ule ule alioutumia kunikashifu na kusema maneno ya Uongo kinyume chahapo nitachukua hatua za kisheria juu yake, aidha ninatafakari njia muafaka za kisheria zakufuata ili jambo hili lifike mwisho. 
Katibu Mkuu (mstaafu) FAT/TFF 

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHMarch 28, 2012 at 7:05 PM

    MICHAEL RUDI KWENYE CRICKET NDUGU YANGU AMBAKO NAKO UADILIFU NADHANI UNAHITAJIKA PIA...!

    HAKUNA ANAYEWEZA KUKUTAKASA UKARUDI KWENYE MPIRA,UNAPOTEZA MUDA.

    MBONA WEWE ULIWAHI KUGOMBEA UKATIBU UENEZI WA CCM DAR NA KUSHINDWA NA HAJI SUNDAY?INA MAANA WATU WAWAPONGEZE WANA CCM DAR KWA KUKUNYIMA KURA AU?

    NA PIA WEWE SI UMEWAHI KUGOMBEA UBUNGE HUKO KWENU AMBAPO PIA KATIKA UCHAGUZI WA NDANI WA CCM KURA HAZIKUTOSHA,VIPI TUWAPONGEZE WANA CCM AGAIN KWA KUKUNYIMA KURA KWA KUKOSA UADILIFU AU?

    MDAU WA BOMBA.REVERE,BOSTON,MASACHUSSETTS.

    ReplyDelete

Post a Comment