'MPENZI CHOCOLATE' YAWAACHA HOI ES SETIF


WIMBO  ‘Mpenzi Chocolate’, ulioimbwa na kundi la muziki wa mipasho la Jahazi Modern Taarab, la jijini Dar es Salaam chini ya Mfalme  Mzee Yusuf, umekuwa kiburudisho cha nguvu kwa wachezaji wa timu ya Es Setif ya Algeria.
Katika kuthibitisha kuwa wimbo huo unawaliza wachezaji hao walimuomba dereva wa gari linalowabeba aina ya Nissan Civilian min Bus na T 413 BXN, kuwawekea wimbo huo wakati wakitoka kwenye mazoezi ya  leo asubuhi kwenye uwanja wa Karume.
Mara baada ya dereva huyo kuwawekea wimbo huo wenye wachezaji hao walianza kupiga mbinja na makofi wakishangilia jambo lililoonesha kuwa wimbo huo umewakuna vilivyo.
“Hawa wachezaji hata wakati wakija hapa uwanjani asubuhi walikuwa wakipiga makofi huku wakishangilia wimbo wa taarbu uliokuwa ukipigwa kwenye gari lao lakini mimi sikuusikia wimbo wenyewe,” alisema mmoja wa mashuhuda.

Comments