MOURINHO AELEZEA HISIA ZAKE KUHUSU ABIDAL


Abidal
KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho leo ameelezea masikitiko yake juu ya beki wa Barcelona, Mfaransa Eric Abadal, ambaye alikuwa ana uvimbe kwenye ini mwaka mmoja uliopita, lakini sasa anatakiwa upasuaji kamili wa ini.
Mourinho amesema hali ya afya ya Abidal imewagusa hata wachezaji wa timu yake ambao wanamuombea dua njema mchezaji huyo.
“Ni moja ya mambo kama hayo yanayofuta tofauti baina ya klabu," alisem kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari leo kuelekea mechi kati ya Real na Malaga kesho.
"Kama tunaweza kuonyesha sapoti yetu ya wazui kwa njia yoyote, wachezaji wetu watafanya hivyo kesho."
Barcelona ilisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, Abidal anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa iniwiki zijazo, jambo ambalo linaweka shakani mustakabali wake wa kucheza Kombe la Mataifa ya Ulaya mwaka huu au hata soka ya ushindani tena.
Kama alivyosema kocha wa wapinzani wake, Barca, Pep Guardiola, Mourinho alisema angependa kumuona tena mchezaji huyo anarejea uwanjani baada ya kufanyiwa operesheni.
“Kama anaweza kucheza tena katika kiwango cha juu, wote tutafurahia hilo. Lakini jambo la msingi ni kwamba, kumtakia maisha marefu na ya furaha.

Comments