Mkutano Mkuu wa kawaida wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) uliokuwa ufanyike Machi 24 na 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam
umesogezwa mbele hadi Aprili 21 na 22 mwaka huu.
Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Machi 10 mwaka huu
jijini Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Rais Leodegar Tenga uliamua kusogeza
mbele Mkutano Mkuu kutokana na mtiririko wa matukio ndani ya TFF katika kipindi
hicho.
Ajenda katika Mkutano Mkuu huo wa kawaida wa TFF kufungua
kikao, kuthibitishwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, kuthibitisha muhtasari wa
Mkutano Mkuu uliopita, yatokanayo na muhtasari wa kikao kilichopita, hotuba ya
Rais, kupokea taarifa za utekelezaji za wanachama na kupokea taarifa ya
utekelezaji ya Kamati ya Utendaji.
Nyingine ni kupitisha taarifa ya ukaguzi wa hesabu za mwaka
uliopita, kupitisha taarifa ya wakaguzi wa hesabu na hatua zilizochukuliwa,
kupitisha bajeti ya mwaka 2012, kupitisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba
ya TFF, kujadili mapendekezo yaliyowasilishwa na Wanachama au Kamati ya
Utendaji, mengineo na kufunga kikao.
Comments
Post a Comment