MILIONI 72 ZAPATIKANA YANGA NA AZAM



Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Azam lililochezwa Machi 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 72,731,000. 
Jumla ya watazamaji 19,339 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000 viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati kwa VIP A ilikuwa sh. 15,000. 
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 11,303,932.20 kila timu ilipata sh. 14,726,592.20, uwanja sh. 4,908,864.07. 
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,963,545.63, TFF sh. 4,908,864.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,454,432.03, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 490,886.41 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 4,908,864.07.
 Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. waamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, tiketi sh. 3,540,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000. 
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata tena sh. 1,353,730 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata tena sh. 1,160,340. 

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Comments