MICHAEL WAMBURA KUJIBU MAPIGO YA TFF



ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Michael Wambura amesema anajipanga kujibu mapigo kuhusiana na taarifa dhidi yake zilizotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deogratius Lyato.

Akizungumza na mamapipiro blog kwa simu jana, Wambura alisema kuwa kwa sasa yupo nje ya nchi na pindi atakaporejea atasoma kwa undani taarifa ya Lyato kabla ya kujibu mapigo.

"Dada nimesikia huko Lyato ametoa taarifa kuhusiana na masuala mbalimbali ikiwemo masuala yangu...mimi nashangaa ni kwa nini wanashindwa kuelezea hoja husika na badala yake kukaa na kunijadili mimi?...ngoja nitakaporejea huko nitaweka mambo hadharani", Alisema Wambura

Baadhi ya maamuzi ya kamati ya uchaguzi yaliyotolewa na Lyato kuhusiana na Wambura ni pamoja na sakata la Uchaguzi mkuu TFF wa mwaka 2008 na kusema kuwa walimuengua Wambura kugombea nafasi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa TFF kwa kutokidhi matakwa ya uadilifu kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF. 
            Jingine ni maamuuzi ya mkutano mkuu wa TFF  katika kikao chake mwaka 2007 kilipitia ripoti za ukaguzi wa mahesabu ya FAT/TFF kwa kipindi cha mwaka 2002 hadi 2004 na baada ya kujiridhisha kuhusu ubadhirifu uliofanywa na uliamua afikishwe kwenye vyombo vya dola kwa ubadhirifu wa fedha za FAT/TFF alioufanya kama ilivyoainishwa kwenye ripoti za ukaguzi wa Mahesabu. Sekretarieti ya TFF mwaka 2007 ikitekeleza maagizo ya Mkutano Mkuu wa TFF na suala hilo lilpelekwa Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi ilithibitisha maombi ya TFF kwa barua  yake ya tarehe 18 Januari 2008 na kumfungulia jalada  Ndg Michael Wambura kwa kosa la wizi  akiwa Mtumishi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF inaheshimu maamuzi ya Mkutano Mkuu wa TFF na hadi sasa haijataarifiwa kwa maandishi na chombo chochote kama suala hilo limefikia ukomo wa aina yoyote.
 
     Pia katika uchaguzi wa Simba mwaka 2010 Wambura aliomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti  Hata hivyo alikatiwa rufaa na Ndg. Daniel T. Kamna  kwa kutotimiza matakwa ya Ibara ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF kama ilivyoamuliwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na pia Kamati ya Rufaa ya TFF mwaka 2008 wakati alipoomba kugombea nafasi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa TFF. Kamati ilikubaliana na maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi na Kamati ya Rufaa ya TFF mwaka 2008 kwamba Bw. Michael R. Wambura  si mwadilifu  kama ilivyonyeshwa kwenye aya ya 2.1 na 2.2 hapo juu na hivyo hakukidhi matakwa ya Ibara ya 29(7) ya Katiba ya TFF na Ibara ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF.  Kamati ilimuondoa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Simba SC.
 
            
3.                   MAAMUZI KUHUSU UCHAGUZI WA FAM
 
            Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilimuondoa Ndg. Michael Wambura kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa FAM kwa kuwa alifungua kesi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba akiwa ni mwanachama wa Klabu ya Simba kuzuia uchaguzi wa klabu ya Simba usifanyike, jambo ambalo ni uvunjaji wa Katiba ya Klabu ya Simba, ukiukwaji wa Katiba ya FAM, TFF na FIFA.
 
            Pia, Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliweka wazi kama ilivyobainisha kwenye uchaguzi wa Klabu ya Simba kwamba suala la uadilifu wa Ndg. Wambura lilishafanyiwa maamuzi na Kamati ya Rufaa ya TFF mwaka 2008 kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi Mkuu wa TFF. Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi huo na Katiba ya TFF Mamlaka pekee inayoweza kutengua uamuzi huo ni Mahakama ya Usuluhishi wa masuala ya Michezo (CAS) iliyo na makao yake Lausanne , Switzerland .
 
           

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHMarch 8, 2012 at 1:57 AM

    michael wewe sasa hivi mimi ningekushauri urudi kwenye "kriketi"soka basi tena,wewe ulipewa nafasi tena ukijua kabisa wewe hukua mtu wa mpira bahati mbaya ukai abuse kwa kukosa uadilifu na hukua na kigezo cha elimu.Kwa sasa najua elimu unayo ya kutosha na uishukuru tff kukufanya urudi shule,hii elimu itakusaidia sana maishani.

    lakini mpira unataka watu waadilifu wewe huna sifa hiyo na bahati mbaya huwezi kusomea uadilifu,bora ukae pembeni na kurejea kwenye viunga vya upanga kwa mzee zuri remtullah mkashirikiane kuendeleza mchezo wenu wa kriketi ambao umelega lega sana.

    mdau wa yanga bomba uhuru branch,Revere,Masachussets.usa.

    ReplyDelete

Post a Comment