Meneja masoko wa maonyesho ya Harusi K Omary (kati )akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) kuhusiana na maonyesho hayo kushoto kwake ni mmoja ya washiriki wa maonyesho hayo Nicole na kulia ni ofisa habari wa maonyesho hayo Amisa Juma
Kwa awamu
ya tatu maandalizi ya maonyesho ya
Harusi yanayotarajia kufanyika tarehe 30 machi hadi 1 april katika ukumbi wa
Diamond Jubilee yatakua na washiriki na
wadau mbalimbali waliobobea kwenye maswala ya Harusi pamoja na mahitaji yote ya
Harusi.
Muanzilishi na muandaaji wa maonyeshao haya ya
kila mwaka Mustafa Hassanali alisema“
Maonyesho ya mwaka huu yatakua makubwa sana kulinganisha na ya mwaka jana na
tunatazamia kuyafanya maonyesho haya ya Harusi kuwa maonyesho makubwa nchini
kote miaka ijayo”.
Ukweli
katika nukuu, Maonyesho haya ya Harusi yalowavutia zaidi ya wafanya maonyesho
40 waliothibitisha ushiriki wao,wengi
wakiwa waliwahi kushiriki katika miaka iliyopita ,wameweza kuona ukuaji katika
maonyesho haya.
“ Harusi
inaleta umoja katika familia na jamii na ni moja kati ya nyakati pekee
zinazotokea katika maisha,hivyo mpango wetu ni kutoa mahitaji ya bibi Harusi na
bwana Harusi katika sehemu moja.na huu ni wakati muafaka wa wao kujipatia
uzoefu katika bidhaa na huduma zote harusi,” alisema meneja masoko Hamis K
Omary.
Maonyesho
ya Harusi yanaleta pamoja wadau na wachuuzi mbalimbali waliobobea katika maswala ya
Harusi na kufanya maonyesho haya kuwa na
kiwango na uhakika nchini Tanzania . Kati ya
wachuuzi mbalimbali watakaoshiriki mwaka huu ni wachuuzi wa keki, maua , wapiga picha, gauni za
harusi, tovuti za wabunifu wa harusi, pamoja
ubunifu mbalimbali unaousiana na maswala mazima ya harusi.
Mmoja kati ya washiriki katika maonyesho y
Harusi 2012, ni Gabriel Makupa wa GRM productions, ambae ni mtayarishaji maarufu wa picha mbalimbali za Harusi. “
Tumepata uzoefu mzuri kwa mwaka ulopita ulotusaidia kupata wateja na nafasi ya
kukuza biashara. Tulitangaza bidhaa na
huduma zetu na kukuza idadi ya wateja kwenye maonyesho ya Harusi 2010 na ndio
maana tunashiriki kuanzia kipindi hicho.
Kuna nafasi
chache tu ambazo zinapatikana katika maonyesho ya mwaka huu.“Mpaka sasa
makampuni 40 yanayohusika na maswala mbalimbali ya Harusi yamedhibitisha
ushiriki wao na tunatarajia idaidi ya washiriki kuongezeka.So far 40 wedding
related. Mwaka huu tuna bidhaa mpya kabisa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo
ili na wao waweza kukua.kwa hivyo tunawaomba wale wote wanaohusika na maswala
ya Harusi kushiriki katika maonyesho haya ya Harusi” alimalizia Bw. Omary
Ikiwa ni
msimu wa Harusi katika kipindi hiki cha
pasaka, maonyesho haya ya Harusi si
yakukosa kwa familia, marafiki,na wanakamati wa Harusi.huu ni wakati wa kupata
vipaji vya ubunifu katika mambo yote ya Harusi.
Maonyesho ya Harusi 2012 ni bure kwa watu wote kuhudhuria
Maonyesho ya Harusi 2012 yamedhaminiwa Clouds FM, Clouds TV, The Citizen, Global
Outdoor Systems, 2M Media, Ultimate Security, Vayle Springs, Eventlites, MH
Gallery, Dar411, Epidor na 361 degrees.
Comments
Post a Comment