MAZZARRI ATAKAA KWENYE BENCHI KESHO


KOCHA wa Napoli, Walter Mazzarri atakaa kwenye benchi kesho kuiongoza klabu yake katika mechi ya marudiano, hatua ya 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea, baada ya Mahakama ya Usuluhishi ya FIFA kusitisha adhabu yake ya kukosa mechi ya pili, imesema taarifa ya klabu hiyo leo.
Mazzarri alikosa mechi ya kwanza dhidi ya Chelsea ambayo Napoli ilishinda 3-1, baada ya Uefa kumfungia mechi mbili kwa kumsukuma mpinzani wake katika mechi dhidi ya Villarreal.
Kocha huyo maarufu Serie A kwa mkato wake wa nywele, amefanya kazi kubwa kuirudisha kwenye chati klabu hiyo ya Naples na kesho atakuwa na mtihani kwenye Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Stamford Bridge ambao akifanikiwa sambamba na Inter Milan ambao watamenyana na Olympique Marseille ya Ufaransa, ina maana Italia itaingiza timu tatu Robo Fainali na England watakuwa kapa.


Comments