NYOTA
wa soka nchini India, amefariki dunia baada ya kupatwa na ugonjwa wa moyo
akiwa katika mechi ya Ligi ya Shirikisho la Soka la India ngazi ya Wilaya ya
Bangalore, Kusini mwa Jiji la Bangalore.
Aliyefariki
dunia ni kiungo D. Venkatesh, 27, wa Bangalore Mars, ambaye aliingia akitokea
benchi dakika ya 73 na kudondoka mwishoni mwa mechi hiyo, dhidi ya klabu ya
South Western Railway.
Vyombo
vya habari nchini India vimeripoti leo kuwa wakati mechi hiyo
ikichezwa kulikuwa hakuna gari la wagonjwa uwanjani hapo na Venkatesh
alifikishwa katika Hospitali ya Hosmat kwa kutumia baiskeli ya matairi matatu
‘Guta’.
Uchunguzi
wa awali unaonesha kuwa sababu za kifo cha nyota huyo ni ugonjwa wa moyo.
Gazeti
la The Times nchini India, lilimkariri Dk. Ajith Benedict Royan wa Hospitali ya
Hosmat, akisema kuwa hakukuwa na majeraha yoyote ya nje yalioonekana katika
mwisli wa Venkatesh, yanayoweza kuwa kama sababu ya kifo cha ghafla cha
mchezaji huyo.
“Labda
kama angetundikiwa oksijeni au matibabu sahihi wakati wa tukio, ingesaidia
kuokoa moyo kusimama,” gazeti hilo lilimkariri Royan akisema.
Shirikisho
la Soka la India kwa ngazi zote (AIFF) limethibitisha kutokea kwa kifo cha
mchezaji huyo na katika maelezo yake kikasema: “AIFF inamuombea Venkatesh
apumzike kwa amani.”
Comments
Post a Comment