MAN UNITED MWENDO MDUNDO


MABAO mawili ya Javier Hernandez ‘Chicharito’ yalikuwa bonge la mchango wakati Manchester United ikiwafunga Wolverhampton Wanderers mabao 5-0 jioni hii.
Ushindi huo dhidi ya Wolves iliyocheza sehemu kubwa ya mchezo ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja, inawafanya United wazidi kujitanua kileleni mwa Ligi Kuu  na kujifariji pia baada ya kutupiwa virago kwenye michuano ya Ulaya.
Pamoja na mabao ya mpachika mabao huyo wa ki- Mexico, wengine waliozoidi kuichimbia kaburi Wolves iliyo kwenye hatari ya kushuka daraja ni Jonny Evans, Antonio Valencia na Danny Welbeck.
Beki wa Wolves, Mfaransa Ronald Zubar alilimwa kadi ya pili ya njano dakika ya 40, wakati United wakiwa wanaongoza 1-0.
United sasa ipo kileleni kwa pointi nne zaidi dhidi ya mahasimu wao, Manchester City, ambao hata hivyo wako nyuma kwa mchezo mmoja. Manchester City pia wametolewa Europa League Alhamisi.

Comments